July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nyalandu atinga kwenye mdahalo kwa chopa, azomewa

Spread the love

WAZIRI wa Malialisili na Utalii na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amezomewa na wananchi kwenye mdahalo uliofanyika Ukumbi wa parokia ya Ilongero 11 Oktoba mwaka huu. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Wakizungumza kwa simu na MwanaHalisi Online kwa simu toka Singida watu waliohudhuria mdahalo huo unaoratibiwa na Azam Tv katika kipindi chake cha panga pangua, wamesimulia kwa Nyalandu alizomewa sababu alizungumza uongo.

Kipindi hicho cha panga pangua ambacho kitarushwa kupitia Azam TV, kiliwakutanisha Lazaro Nyalandu wa CCM na David Djumbe anayegombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendele (Chadema).

Nyalandu alifika katika kijiji cha Ilongero kwa kutumia helkopta kuhudhuria mdahalo huo uliohusu sera na ilani za vyama na namna watakavyokabiliana na changamoto za Miuondombinu, sekta ya maji, umeme n.k.

Ni katika majibu hayo ambapo Nyalandu alikataa kufuta michango ya shule, na kuanza kukisifu Chama cha Mapinduzi badala ya kuzungumzia changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Mwanahalisi Online, lilipomtafuta Nyalandu hakupokea simu hata baada ya kuandikiwa ujumbe hakujibu.

Nyalandu anayegombea Ubunge kwa awamu nyingine anadaiwa kuwa na mahusiano mabaya na baadhi ya wananchi wa jimbo lake. Ilidaiwa kuwa Aprili 11 mwaka 2012, saa 6:00 usiku katika kijiji cha Mwanyonye, Nyalandu na watu wengine waliotajwa kuwa nao ni Elia Digha pamoja na Reuben walifika na gari No. T.505 BKM, aina ya VX, walikuta kizuizi kilichowekwa na serikali kwa ajili kukagua mazao ya wanyama na misitu, walishuka na kuwatishia walinzi kwa bastola, wakavunja kizuizi, na kuondoka na taa ambayo walinzi hao waliitumia. Baada ya tukio hilo Wanakijiji wa Mwanyonye walipiga simu kijiji kinachofuata.

Kijiji kinachofuata ni Kinyeto, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kinyeto na walinzi walijizatiti ili wazuie ile gari itakapofika, walipofika mtu mmoja alishuka kwenye gari haraka akiwa amenyoosha bastola na kuwauliza walinzi mnafungua au hamfungui, walikataliwa, wakavunja kizuizi.

Haijulikani Nyalandu alikuwa anatorosha nini katika mazingira hayo. Ila walinzi walipopiga picha gari hiyo, na kuchukua namba za usajili, waliripoti polisi mapema kufungua jalada SI/IR/1570/2012 , Kamanda wa polisi Mkoa wa Singida hakupatikana kuzungumzia tuhuma hizi zilitatuliwa vipi hadi sasa.

error: Content is protected !!