Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nyalandu amnasihi Mbowe
Habari za Siasa

Nyalandu amnasihi Mbowe

Lazaro Nyalandu
Spread the love

 

LAZARO Nyalandu, aliyerejea Chama Cha Mapinduzi (CCM), amemshauri, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutoweka masharti magumu ya kwenda kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya Rais Samia, kukubali barua ya Mbowe ya kuomba kukutana naye ili kuzungumza masuala mbalimbali hususan ya kukuza demokrasia na utawala bora.

Nyalandu aliyerejea CCM, tarehe 30 Aprili 2021, akitoka Chadema alikokuwa mwenyekiti wa chama hicho, Kanda ya Kati, ametoa ushauri huo, leo Jumatatu 3 Mei 2021.

Alikuwa akihojiwa katika kipindi cha Clouds360 cha Clouds Televisheni.

Lazaro Nyalandu

“Nawasihi Chadema, waache kuweka masharti magumu ya kuonana na Rais, mkuu wa nchi akitaka kukuona usiweke masharti,” amesema Nyalandu, aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii, katika utawala wa Jakaya Kikwete.

Katika kusisitiza hilo, Nyalandu amesema “wekeni masharti pembeni, nendeni mkamsikilize, nchi hii ina Rais mmoja.”

Akijibu swali aliloulizwa, iwapo akikutana na Mbowe kwa sasa, atamwambia nini, Nyalandu amesema “nitamchukua tukanywe kahana.”

Amesema, wakiwa kwenye kahaha nitamwambia “wasimwekee masharti, waende wakakutane na Rais ili wamsikilize.”

Tarehe 22 Aprili 2021, Rais Samia akilihutubia Bunge la Tanzania, alisema anakusudia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa ili kujadiliana nao masuala mbalimbali yenye maslahi mapana na nchi.

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, katika ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, alisema baada ya Rais Samia kukubali ombi la Mbowe, wanasubiri kupangiwa siku ya kwenda kuonana naye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!