December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nusura ya MV. Nyerere kutokea Mafia

Usafiri hatarishi Mafia

Spread the love

IKIWA ni miezi minne tangu Tanzania kupoteza zaidi ya watu 200 katika Ziwa Victoria kwenye ajali ya MV. Nyerere, watu 75 wamenusurika kufa katika Bahari ya Hindi wakienda kisiwani Mafia. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya injini ya boti waliyokuwa wakisafiria kupata hitilafu na kusababisha boti hiyo kupoteza mwelekeo.

Akizungumzia tukio hilo jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji, Envence Mwijage amesema kuwa, tukio hilo lingesababisha kupoteza maisha ya watu wengi.

Amesema kuwa, jeshi hilo likiwa kwenye doria limeweza kuokoa watu hao wakisubiri hatma yao baharini.

“Boti hii ilitaka kutuharibia sikuu yetu kwamba isingekuwa salama…tumeshrikiana na Wakala wa Meli na wameikagua boti hiyo na sasa imefungiwa kufanya safari mpaka itakapofanyiwa marekebisho,” amesema Kamanda Mwijage.

Kamanda Mwijage amesema kuwa, boti hiyo ambayo hakuitaja jina haitaruhusiwa kufanya safari yoyote mpaka ikaguliwe tena baada ya kutoka kwenye matengenezo kama ilivyoamrishwa.

“Wakishairekebisha, boti hii haitaruhusiwa kuingie kwenye maji na kuanza kazi zake mpaka ipelekwe ikakaguliwe na mamlaka ya kwara nyingine na kisha ipewe kibali.

“Hii maana yake si kwenda kurekebisha tu na kuirejesha kazini, la! Lazima ipate kibali upya,” amesema Kamanda Mwijage.

error: Content is protected !!