Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti
Habari Mchanganyiko

NSSF yawapa darasa wahariri uwekezaji wa nyumba, yapewa cheti

Spread the love

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa wito kwa Watanzania kuchangamkia nyumba na viwanja vinavyouzwa na mfuko kwa njia mbalimbali ili kujikomboa kimaisha. Anaripoti Gabriel Mushi, Morogoro….(endelea).

Wito huo umetolewa jana na Afisa Milki Mkuu, Weraisaria Mushi wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano wa mwaka wa 12 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika mjini Morogoro.

Afisa Milki, Mary Semali kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), akitoa mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu uwekezaji wa mfuko huo kwenye nyumba, viwanja na majengo yanayotoa huduma za hoteli.

Alisema lengo la NSSF ni kuhakikisha mwanachama wa mfuko huo anafaidika na uwekezaji wake vivyo hivyo hata kwa wale ambao si wanachama wa mfuko huo ili kuacha kujitengenezea mazingira ya kuwa ombaomba mtu afikiapo uzee.

 Akifafanua kwa kina kuhusu miradi hiyo uwekezaji, Afisa Milki, Mary  Semali amesema nyumba za makazi zenye viwango na hadhi mbalimbali zipo katika maeneo ya Mtoni Kijichi, Tuangoma, Dungu jijini Dar es Salaam huku viwanja vikiwa upande wa Kibaha mkoani Pwani.

 Amesema nyumba 85 ambazo ni za bei za chini zilijengwa mwaka 2008 kwa awamu ya kwanza katika eneo la Mtoni Kijichi, awamu ya pili zilijengwa 212 mwaka 2011.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Deodatus Balile (kushoto) akimkabidhi Afisa Milki Mkuu, Weraisaria Mushi
cheti cha utambuzi wa mchango wa NSSF kwa Jukwaa hilo. Katikati ni Mjumbe wa TEF, Joseph Kulangwa.

 “Nyumba hizo zina riba ya asilimia 11.4 kwa mwaka na zinatofautiana bei kwani zinaanzia Sh milioni 77 mpaka milioni 133.

 Alisema bei hizo zinatokana na mfumo wa malipo aina tatu ambapo, mtu anaweza kununua nyumba hizo kwa kulipa fedha taslimu, mfumo wa pili mnunuzi anatakiwa kulipia asilimia 10 kisha anamalizia kulipa kwa awamu kwa muda wa zaidi ya miaka 15 wakati mfumo wa tatu mnunuzi anakwenda benki kukopa mkopo wa nyumba ambapo benki humlipia fedha yote kisha kuchukua hati ya nyumba na baada ya mnunuzi kumaliza mkopo wake, benki hurejeshwa hati hiyo.

 Aliongeza kuwa mkopo wa nyumba pia ni nafuu kwa mnunuzi kwani baadhi ya benki zinatoza riba ya asilimia 8.5 kwa mfanyakazi na asilimia 9.5 kwa mfanyabiashara ilihali NSSF ikiwa ni asilimia 11.4 kwa mwaka.

 Mbali na nyumba hizo za bei ndogo, alisema pia zipo za bei kubwa ikiwamo za ghorofa huku Shirika likiwa limejenga majengo manne yenye huduma za hoteli ambazo zitakapokamilika ujenzi wake zitauzwa kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

 Alitaja hoteli hizo kuwa ni Mzizima iliyopo posta jijini Dar es Salaam, moja ipo Moshi mjini Kilimanjaro wakati hoteli ya mafao pamoja na nyingine ya nyota tano zipo Mwanza.

 Pamoja na mambo mengine katika mkutano, NSSF walipewa cheti cha utambuzi kama mmoja wa wadhamini wakuu wa mkutano huo. Cheti hicho kilikabidhiwa na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile kwa Afisa Milki Mkuu, Weraisaria Mushi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!