July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NSSF kuboresha huduma kwa wateja

Spread the love

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) limeanzisha huduma mpya zinazohusu uboreshaji wa mazingira ya utoaji huduma bora kwa wateja ikiwa ni pamoja na mfumo wa kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama. Anaandika Regina Mkonde.

Pia shirika hilo limeanzisha mfumo wa kupima uridhikaji wa huduma itolewayo kwa mteja likiwa ni kushughulikia malalamiko ya wanachama yanayojitokeza sehemu mbalimbali za utoaji huduma.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Eunice Chiume ambaye ni Ofisa Mkuu Idara ya Masoko na Uhusiano NSSF pia amesema, shirika limejipanga kutimiza lengo lake la utoaji huduma bora za mafao ya jamii katika Bara la Afrika ifikapo mwaka 2020.

“Ili kufanikisha lengo letu la utoaji huduma bora, shirika limeanzisha huduma mbalimbali ambazo zinahusiana na kuboresha mazingira ya utoaji huduma bora kwa wateja,” amesema Chiume na kuongeza;

“Juhudi hizi za shirika zinaenda sambambana dhana ya uwazi na uwajibikaji ili kuwathibitishia wanachama jinsi shirika lilivyojipanga kutoa huduma bora kwa wanachama.”

Kupitia mifumo hiyo, mwanachama na mdau yeyote anaweza kutoa maoni yake juu ya namna alivyohudumiwa na watendaji wa ofisi za NSSF, kulipa michango kupitia mifumo ya simu na kutumia mitandao ya kijamii kutoa maoni yao.

error: Content is protected !!