Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Note Book’ ya mwenzake Mbowe yaibua maswali mahakamani
Habari za SiasaTangulizi

‘Note Book’ ya mwenzake Mbowe yaibua maswali mahakamani

Spread the love

 

MAWAKILI wa utetezi, katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, wamehoji kwa nini shahidi wa Jamhuri, SP Jumanne Malangahe, hajatoa mahakamani daftari ‘Note Book’, alichodai kuwa ni miongoni mwa mali zilizokamatwa nyumbani kwa mshtakiwa wa kwanza, Halfan Hassan Bwire. Anaripoti Regina Mkonde, Dar ea Salaam … (endelea).

Maswali hayo yamehojiwa leo Ijumaa, tarehe 17 Desemba 2021 katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, baada ya SP Malangahe kuomba kutoa mali hizo alizodai kuwa zilikamatwa tarehe 10 Agosti mwaka jana, kama vielelezo vya jamhuri.

Mawakili hao wa utetezi, waliiomba mahakama hiyo mbele ya Jaji Joachim Tiganga, isipokee mali hizo, kwa kuwa hazijafuata mlolongo wa utunzwaji na upokelewaji vilelezo (Chain of Custody), wakidai kuwa hazijakamilika kama zilivyokamatwa kutokana na notebook hiyo kutokuwepo.

Wakili John Mallya amedai kuwa, shahidi huyo hakuleta notebook hiyo kwa kuwa alilenga kuficha ushahidi.

“Ushahidi aliuchukua, leo mahakamani anauficha hajauleta. Kidaftari chekundu ni item namba nane. Sababu hajauleta na wakati anaweka ushahidi wake akasema zote aliziweka katika shangazi kaja akaziweka humo akapelekea kwa Sargent Johnson lakini leo ameuficha, ni maana ya kuchuja ushahidi wa namna hiyo,” amedai Wakili Mallya.

Wakili Mallya alihoji athari gani atazipata mshtakiwa huyo kama notebook imebeba maudhui yanayohusiana na kesi inayomkabili.

“Mahakama yako inayimwa fursa ya kuona notebook inawezakana inasema mali zinazoonekana za kijeshi ni za Twanga Pepeta zinatumika kuchezea ngoma. Labda kuna maelezo kwenye notebook zinaonesha kwa nini hizi sare zimepatikana zilipopatikana. Muulzie swali kama kuna content zikija mahakamani zita-relate na kesi za mshtakiwa,” amedai Wakili Mallya.

Wakili Mallya amedai “what if (nini kama) kulikuwa na justifaication, what if kulikuwa na permision ya JWTZ kumruhusu kukaa na sare hizo? Kwa nini ameificha mahakama yako? hiyo ni contradiction ya evidence (mkanganyiko wa ushahidi).”

“pengine aliona itamharibia kesi yake, kwa nini notebook imeishia njiani haikufika mahakamani ? Labda mashahidi waeleze haikuwa na uhusiano na wao wakasaini kwamba haijachukuliwa, ” amedai Wakili Mallya.

Wakili wa Hassan, Nashon Nkungu, aliiomba mahakama hiyo isikubali kuzipokea mali hizo, kwa kuwa shahidi huyo ameshindwa kueleza mahali ilipo Note Book hiyo.

Wakili Nkungu amedai kuwa, kitendo hicho ni kinyume na matakwa ya kifungu cha 22 (4), cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi, kinachoelekeza Askari Polisi kueleza namna alivyoacha baadhi ya mali alizodai alikamata nyumbani kwa mshtakiwa huyo.

“Kwa kuwa shahidi amekuwa mchumi, mchoyo au mnyimi wa maelezo kwenye upande huo, anaiacha mahakama katika maswali, kufahamu vielelezo vilivyochukuliwa haviwi tenderd mahakamani,” amedai Wakili Nkungu.

Akijibu maswali hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando, amedai shahidi huyo alieleza kwa nini hajakileta mahakamani.

“Kwenye hoja kwamba Notebook ambayo ni item namba nane sababu haikueletwa mahakamani, basi mahakama yako ione kwamba vilelezo hivyo havijaletwa katika hali kama ilivyokuwa hapo awali, kwa vile shahidi hajaeleza ni jinsi gani ambavyo aliondokana na kielelezo hiko, haina mashiko sababu shahidi smeleeza kwa nini leo hajaitoa,” amedai Wakili Kidando.

Wakili Kidando amedai kuaa, kutotolewa kaa notebook hiyo hakuwezi kufanya ushahidi wa SP Malangahe kutiliwa shaka katika hatua ya sasa, hadi pale wakati mahsusi utakapofika.

“Hoja hii inakosa mashiko sababu suala hilo limeelezewa kwenye ushahidi na shahidi huyu vilelezo hivyo hata leo alivyofika mahakamani hapa ameelezea mazingira jinsi gani alivyovileta,” amedai Wakili Kidando na kuongeza:

“Katika mazingira hayo ushahidi huo hauwezi ukatiliwa shaka katika hatua hii, mpaka wakati mahsusi wa kuweza kuibua suala la namna hiyo kuhusiana na chain of custody aidha, by way of cross examination (kwa njia ya maswali ya dodoso).”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!