January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Noorj apewa mtihani mwingine, Wambura azidi kuula TFF

Benchi la Ufundi la Taifa Stars

Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imempa nafasi moja ya mwisho kocha wa timu ya taifa, Mholanzi Mart Nooij juu ya mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Kamati hiyo iliyokuwa na kikao lao Dar es Salaam chini ya Rais wake, Jamal Malinzi imewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya COSAFA.

Baada ya majadiliano ya kina, Kamati iliamua kumpa Mart Nooij changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee na asipofanikisha hilo, mkataba wake utasitishwa mara moja.

Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi.

Aidha, katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopold ‘Tasso’ Mukebezi amerejeshwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa. Mukebezi alikuwa Meneja wa Taifa Stars tangu mwaka 2006 hadi mwaka jana.

Wakati huo huo, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015.

Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano TFF.

TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.

Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.

error: Content is protected !!