March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nondo aibua kikwazo mikopo Chuo Kikuu

Abdul Nondo, Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP)

Spread the love

MWENYEKITI wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini (TSNP), Abdul Nondo amekitaja kikwazo kingine kwenye mikopo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini Rita. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Nondo akizungumza na MwanaHALISI Online amesema kuwa Rita wamekuwa kikwazo kwa mikopo ya wanafunzi kutokana na kuchelewesha kuhakiki taarifa za vyeti vya kuzaliwa za wanafunzi.

Amesema kuchelewa kupitia na kuhakiki taarifa za wanafunzi  kunawanyima fursa ya kupata mikopo kutokana muda kuisha na kwamba dirisha la kuomba mikopo linafungwa Tarehe 15 Mwezi huu.

“Sisi kama Mtandao wa wanafunzi tumeiandikia barua Bodi ya Mikopo kuiomba waongeze muda wa kuomba mikopo kutokana na kuhofia wanafunzi wengi watakosa mikopo kutokana na ucheleweshwaji wa uhakika wa vyeti unaofanywa na  Rita,” amesema Nondo.

Amewatoa hofu wanafunzi waliomba mikopo kuwa hoja ya TSNP ina maslahi kwao hivyo itasikilizwa na kufanyiwa kazi.

error: Content is protected !!