Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yazindua tawi la 227 Mwanza, yasaidia serikali kukusanya trilioni 8.6
Habari Mchanganyiko

NMB yazindua tawi la 227 Mwanza, yasaidia serikali kukusanya trilioni 8.6

Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania imeendelea kujidhatiti kibiashara na kujiimarisha kulihudumia taifa kupitia mtandao wake wa matawi ambao sasa umefikia matawi 227. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Idadi hiyo imefikiwa baada ya uzinduzi wa tawi la NMB Buhongwa mkoani Mwanza jana Jumatano ya tarehe 6 Julai 2022.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (wa pili kushoto) akikata utepe ili kuzindua tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza juzi, wa katikati ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi(kushoto), Meya wa jiji la Mwanza Sima Costantine (wa pili kulia) na Meneja wa NMB kanda ya Ziwa – Baraka Ladslaus wakishuhudia. NMB Imefungua tawi la NMB Nyamagana ambalo ni la 13 Mkoani Mwanza na la 227 Tanzania.

Taasisi hiyo kubwa ya fedha nchini Tanzania imesema pamoja na kuwahudumia wananchi wa eneo hilo, tawi hilo jipya litaongeza mchango wa NMB kwenye ujenzi wa taifa ikiwemo kusaidia kukusanya mapato ya serikali kupitia mifumo yake ya kidijitali.

Akizungumza kabla ya ufunguzi rasmi wa tawi hilo lililopo Wilaya ya Nyamagana, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi, alisema kati ya mwaka 2019 na 2021, NMB iliisaidia serikai kukusanya mapato yenye thamani ya Sh.8.6 trilioni 8.6.

Akifafanua mchango wa NMB katika juhudi za maendeleo za serikali, Mponzi alisema sasa hivi Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) una zaidi ya taasisi 1,100 zilizounga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato.

Aidha alisema pamoja na mtandao mpana wa matawi, NMB imeendelea kutumia tekinolojia kufikisha huduma zake kwa watanzania wengi zaidi na kulihudumia taifa kwa ujumla.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Sauda Msemo (wa tatu kushoto) akikata utepe ili kuzindua tawi la NMB Buhongwa jijini Mwanza juzi, wanne kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi(wa Pili kushoto), Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula (kushoto),Meya wa jiji la Mwanza Sima Costantine (wa pili kulia) na Meneja wa NMB kanda ya Ziwa – Baraka Ladslaus wakishuhudia. NMB Imefungua tawi la NMB Nyamagana ambalo ni la 13 Mkoani Mwanza na la 227 Tanzania.

“Tunazo pia mashine za kutolea fedha yaani ATM zaidi ya 800 nchi nzima, na mawakala zaidi ya 14,600 waliosambaa nchi nzima, hawa wamesaidia sana kusogeza huduma za NMB karibu zaidi na watumiaji,” alisema

“Mafanikio haya yanatokana na ushirikiano wetu mkubwa na Serikali ambaye ni mdau mkubwa kwa benki yetu pamoja na wateja wetu ambao leo ni mashuhuda wa uzinduzi wa tawi la NMB Buhongwa,” alifafanua na kusema wataendelea kushirikiana na wadau wao wote kuimarisha huduma za kifedha nchini.

Mponzi alisema tawi hilo jipya ambalo ni la 13 mkoani Mwanza na 38 Kanda ya Ziwa, ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki, zikiwemo zile za mikopo kama kuwakopesha wakulima kwa riba ya asilimia tisa.

Mtaalam huyo wa NMB alisema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika jitahada za serikali za kuimarisha kilimo nchini.

Kwa mujibu wa Mponzi, tayari benki hiyo imetoa mikopo ya kilimo ya TZS bilioni 100 kwa riba isiyozidi asilimia 10.

“Kiwango hiki tayari kimeisha na sasa tumeongeza TZS bilioni 100 na kushusha  riba hadi asilimia tisa,” alisema

Mponzi alisema michango mingine ya Benki ya NMB kwa Serikali ni pamoja na kutoa gawio la TZS bilioni 30.7 kwa mwezi uliopita na kulipa kodi zenye thamani ya TZS bilioni 269 mwaka 2021.

“Tawi hili la NMB Buhongwa ni tawi kamili lenye huduma zote za kibenki yaani huduma za miamala, mikopo, ushauri, kufungua akaunti, kufanya huduma za kubadiri fedha za kigeni, huduma za bima na hata ushauri wa masuala ya biashara na fedha,” alisema Mponzi

Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo alikuwa ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Sauda Msemo, aliyesema NMB ni mshiriki na mdau muhimu katika juhudi za Serikali za kuboresha huduma za kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta mbalimbaili hasa za elimu na afya.

“Pamoja na kusogeza huduma za kibenki karibu na wananchi hadi vijijini kupitia matawi, vituo vya huduma na mawakala, NMB pia ni mshiriki na mdau muhimu katika juhudi za Serikali za kuboresha huduma za kijamii kwa kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta za alimu na afya,” alisema Sauda

Naibu Gavana huyo aliipongeza NMB kwa kutenga zaidi ya Sh.200 bilioni kwa ajili ya mikopo yenye riba nafuu kwenye sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji huku akiziagiza benki na taasisi zote za fedha nchini kupunguza viwango vya riba ya mikopo kufikia tarakimu moja kuwezesha wananchi kunufaika na uamuzi wa Serikali kupitia BoT wa kupunguza riba za hati fungani.

“Nawapongeza NMB siyo tu kwa kutenga zaidi ya Sh200 bilioni kwa ajili ya mikopo kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, bali pia kwa kupunguza riba kutoka asilimia 10 ya awali hadi asilimia 9,” alisema Sauda

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, Meya wa Jiji la Mwanza, Constantine Sima na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, waliwaomba wafanyabiashara na wakazi wa Mwanza kutumia fursa ya uwepo wa huduma za kibenki kukopa kuongeza tija katika shughuli zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!