Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Biashara NMB yatoa vifaa vya milioni 29 hospitali ya Amana, Shule 3 Dar
Biashara

NMB yatoa vifaa vya milioni 29 hospitali ya Amana, Shule 3 Dar

Spread the love

HOSPITALI ya Rufaa ya Amana na Shule tatu za msingi za Buguruni Kisiwani, Kivule na Airwing zilizoko Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, zimeingia katika orodha ya wanufaika wa Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR 2022) ya Benki ya NMB. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kutokana na kuingia kwenye CSR, juzi Ijumaa ya tarehe 4 Machi 2022, NMB ilikabidhi misaada yenye thamani ya Sh.29 milioni.

Makabidhiano hayo yalifanyika Shule ya Msingi Buguruni Kisiwani, ambako Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Ng’wilabuzu Ludigija, vifaa vyenye thamani hiyo.

Fedha hizo Sh.29 milioni ni kati ya Sh.2.8 bilioni zilizotengwa na benki hiyo kusaidia Sekta za Elimu na Afya kwa mwaka 2022.

Wakati Hospitali ya Amana ikikabidhiwa masanduku ya kuhifadhia vifaa tiba vya wagonjwa waliolazwa ‘bed side rockers’ 30 zenye thamani ya Sh.9.2 milioni, Shule ya Airwing ilikabidhiwa madawati 100 yenye thamani ya Sh.10 milioni huku Shule ya Buguruni Kisiwani ikikabidhiwa mabati 150 yenye thamani ya Sh.4.8 milioni.

Shule ya Msingi Kivule, ilikabidhiwa madawati 50 yenye thamani ya Sh.5 milioni hivyo kufanya jumla kuu ya thamani kufikia Sh.29 milioni.

Akizungumzia msaada huo, DC Ludigija aliishukuru benki hiyo akisema anaamini misaada hiyo inaenda kuamsha ari ya kujisomea na kuboresha mazingira ya kufundishia, pamoja na kuhudumia wagonjwa.

Ludigija aliitaka NMB kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, katika kunyanyua elimu na kuboresha miundombinu ya afya wilayani mwake, ambako uwingi wa shule na hospitali, umesababisha kuongezeka kwa wanafunzi na wagonjwa, hivyo kuongeza changamoto.

“Serikali tunawashukuruni kwa namna mnavyojitoa kutatua changamoto kwenye elimu na afya wilayani Ilala, ambako uhitaji ni mkubwa na bado nguvu ya Serikali haitoshi bila sapoti za wadau. Kwa hili mnadhihirisha ukweli kuwa; ‘Ninyi NMB ni Benki Baba Lao,’ mnaoongoza katika kutekeleza takwa la CSR,” alisema Ludigija.

Kwa upande wake, Donatus aliishukuru Manispaa ya Ilala pamoja na viongozi wa shule zilizokabidhiwa misaada hiyo kwa kuitazama NMB kama mshirika sahihi katika utatuzi wa changamoto, hivyo kuipelekea maombi yao na kwamba wao wanajisikia faraja kuwa wadau vinara katika kurejesha kwa jamii sehemu ya faida yao.

“Misaada hii tunaitoa chini ya mwamvuli wa CSR, programu ya kila mwaka, ambayo kwa mwaka huu wa 2022 tumetenga kiasi cha Sh.2.8 bilioni ambazo ni sawa na asilimia moja ya faida ya benki yetu kwa mwaka uliopita, tukirejesha kwa jamii, ambayo ndio sehemu ya wateja wetu,” alisema na kuongeza:

“Kwa sababu sehemu ya faida tunairudisha kwao, basi wito wetu wa Watanzania ni kutumia huduma zetu zilizotapakaa matawini kote nchini, ambako kuna mikopo ya riba nafuu kwa kada zote za wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara, wajasiriamali, wafugaji na wavuvi. NMB ndio suluhu ya changamoto za kifedha,” alisisitiza Donatus.

Awali, akisoma risala ya shule kwa Mkuu wa Wilaya, Mwalimu Lilian Saguti wa Shule ya Buguruni Kisiwani, alisema shule hiyo iliyoanzishwa miaka 19 iliyopita (2003), kwa sasa ina wanafunzi 1,169 na walimu 32 huku ikikabiliwa na changamoto za madawati, viti na meza za walimu, pamoja na vifaa vya michezo, ikiwemo viwanja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Biashara

Black Gold kasino mgodi wa madini Meridianbet 

Spread the love  Dhahabu ni moja kati ya utajiri wenye thamani kubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!