Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Biashara NMB yatangaza ufadhili wa wanafunzi 2022
Biashara

NMB yatangaza ufadhili wa wanafunzi 2022

Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa amekabidhi viti na Meza kwa Shule ya Sekondari ya Mwanalugali ya mkoani Pwani wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Sita ya Shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo.
Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania inatarajia kutoa ufadhili kwa wanafunzi 200 ambapo wanafunzi 150 ni wa kidato cha tano na sita huku 50 kwa vyuo vikuu kwa mwaka 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kibaha…(endelea).

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Mkaguzi wa ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa wakati wa mahafali ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Mwanalugali iliyopo wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Baragomwa alisema mwaka jana NMB ilizindua asasi ya kiraia inayoitwa NMB Foundation ambapo kuna kitu kinaitwa Nuru Yangu Scholarship na Mentorship Program ambayo inatoa ufadhili wa masomo.

Aidha, NMB imetoa viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya Sh.5 milioni kwenye Shule ya Sekondari ya Mwanalugali kwa ajili ya kupunguza changamoto za shule hiyo.

“Ufadhili huu ni wa masomo kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na kwa wale wanaoingia vyuoni kigezo kikubwa uwe umefaulu vizuri na pia wanaotaka familia duni,” alisema Baragomwa.

Alisema anaamini wahitimu wote hawa wataendelea na masomo katika vyuo vikuu washike masomo na wasome kwa bidii sana vijana kwani siku hizi vijana wamejenga dhana kuwa elimu bora inapatikana nje ya nchi yaani majuu ambapo hiyo ni dhana potofu, elimu ya Tanzania ni bora sana na tujivunie.

“Kwa taarifa yenu tu mimi pia ni zao la elimu hii hii na nilisoma katika shule kama hizi na nilizingatia vyema mafundisho ya walimu wangu na wazazi na mpaka leo hii nipo hapa kama mgeni rasmi nikiwa ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB ni benki kubwa na inaendelea kupanuka kila kukicha tunategemea kupitia wahitimu hawa tutapata wafanyakazi bora kabisa watakaoyaendeleza yale yanayofanywa hii leo tena kwa kutumia sayansi na teknolojia ya juu kabisa,” alisema Baragomwa.

Alisema wanahamasisha wanafunzi wasome kwa bidii na kwa kufanya hivyo Taifa litapata wakina Benedicto Baragomwa, wakina Kassim Majaliwa (waziri mkuu) na wa kina Philip Mpango (makamu wa Rais) na kuwataka walimu kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia vijana kuinua kiwango cha elimu, kufanya kazi kwa bidi kutatoa mchango mkubwa hasa katika kuitikia wito wa Serikali wa kuboresha elimu.

“Wanafunzi wanapomaliza shule na kuingia mtaani, wakumbuke kuna hatari ambazo wasipokuwa makini, watajikuta wanatumbukia katika majanga mbalimbali yanayoweza kukiangamiza kizazi cha vijana.

Mfano Ugonjwa wa UKIMWI na Madawa ya kulevya; ukizingatia ukweli kwamba, Taifa la watu dhaifu kiafya, haliwezi kupambana na umaskini,” alisema Baragomwa.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Joseph Mkumbo alisema changamoto kubwa iliyopo ni kutokuwa na uzio hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi hasa wavulana kutokana maeneo mengi kutoendelezwa na kusababisha matokeo kuwa mabaya.

Mkumbo alisema changamoto nyingine ni upungufu wa samani meza uchakavu wa sakafu milango na madarasa na malengo ni kuwa uzio ifikapo Julai mwaka huu ili kudhibiti utoro.Shule hiyo ilianza mwaka 2007 na kidato cha tano kilianza mwaka 2020 na wamehitimu 32.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari

Bosi utalii atoa ujumbe wa mikopo nafuu ya NMB

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini...

BiasharaHabari

NMB yavutia wabunifu suluhisho za kifedha, Dk. Mpango agusia vijana

Spread the love  MFUMO wa majaribio wa suluhishi za kifedha ulioandaliwa na...

BiasharaHabari

NMB Nuru Yangu yazinduliwa, 200 kunufaika

Spread the loveBENKI ya NMB nchini Tanzania imetangaza rasmi kuanza kupokea maombi...

BiasharaHabari

Waziri Bashe uso kwa uso vigogo NMB bungeni

Spread the loveWAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe amekutana na kufanya...

error: Content is protected !!