Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yashiriki Kongamano la kwanza Kigoda cha Utafiti cha Mkapa
Habari Mchanganyiko

NMB yashiriki Kongamano la kwanza Kigoda cha Utafiti cha Mkapa

Spread the love

BENKI ya NMB imepongeza uanzishwaji wa kongamano la Kigoda cha utafiti cha Mkapa na Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT). Kwani hiyo ni njia njema ya kuenzi uzalendo na utumishi mwema wa Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin William Mkapa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Hayo yalisemwa na Kaimu meneja wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa, Dickson Richard wakati wa uzinduzi wa Kigoda hicho katika ukumbi wa M15 kwenye Chuo kikuu cha mtakatifu Agustine(SAUT) kampasi ya Mwanza.

Richard alisema katika uzinduzi wa kigoda cha mkapa benki yao imeshiriki katika kuenzi kumbukumbu za kuzaliwa kwake. Alisema benki ya NMB ipo katika kuwekeza na kufanya mashirikiano na Jumuiya kama SAUT katika kuboresha yaliofanya na wasisi wa nchi yetu.

‘’Benki ya NMB ni zao la sera ya ubinafisishwaji ya Hayati Rais Benjamin Mkapa. Hivyo Rais Mkapa ni chachu ya hatua zote kubwa ambazo benki ya NMB imekuwa ikizipiga na hata kukua na kuwa benki kubwa kama ilivyo sasa,” alisema Richard.

‘’Hayati Mkapa alikuwa kiongozi aliyekuw anasaidia watu wa kipato cha chini, na sisi kama Benki tunathamini Jamii zilizotuzunguka na kutatua changamoto zinazowakabili hususani katika sekta ya Elimu na Afya. Na kwa mwaka huu wanafunzi 100 watapatiwa ufadhili wa masomo ya chuo kikuu kupitia programu yetu ya NMB Nuru yangu Scholarship,” alisema Richard.

Naye makamu mkuu wa Chuo cha mtakatifu Agustine (SAUT) kampasi ya Mwanza, Profesa Costa Mahalu ameishukuru benki ya NMB kwa kudhamini kongamano hilo la Mkapa.

Profesa Mahalu alisema Hayati Mkapa alichangia kwa asilimia kubwa kwa upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo binafsi. Amesema Hayati Mkapa aliisaidia sana Chuo cha SAUT kupatiwa eneo la kujenga chuo hicho mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Uongozi Balozi Ombeni Sefue watanzania kujenga utaratibu wa kujisomea vitabu ikiwa kama sehemu ya kumuenzi aliekuwa Rais mstafu wa awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa.

“Watanzania inatakiwa tusome vitabu katika kumuenzi hayati Benjamin Mkapa na ukiwa kiongozi usomaji wa vitabu  vinaweza kukusaidia na kuwa mshauri wako mkubwa” alisema Balozi Sefue.

Aliwataka watanzania kusoma vitabu na wasisome vitabu  tu kwa kuwa wanataka kuwa viongozi. Amesema marais wastafu Ally Hassan Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa na Hayati Julius Nyerere walikuwa waumini wakubwa wa kusoma vitabu. Balozi Sefue amewataka Wanafunzi wa Chuo cha kikuu SAUT wasisome kufaulu tu mitihani bali wasome kupanua upeo wa kujua mambo mengi zaidi.

Aliwataka viongozi mbali mbali nchini kusoma vitabu ili waweze kujiamini na kujua mambo mengi zaidi.

Naye mke wa Hayati Mama Anna Mkapa alisema hayati Mkapa alitumia vitabu katika kuongoza taifa letu na alipenda kujifunza kupitia vitabu na kuandika hotuba kwa kutumia vitabu.

Amewataka watanzania wote waendelee kumuombea Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika kuijenga Tanzania mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!