Friday , 1 March 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang
Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the love

Waathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza ndugu zao, makazi, pamoja na mali, wamepatiwa misaada ya kibinadamu na Benki ya NMB. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Misaada hiyo inajumuisha magodoro, vyakula na vifaa vingine, ikiwa lengo ni kutoa msaada muhimu baada ya janga hilo.

Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus (aliyevaa fulana nyeupe), akikabidhi Mbunge wa Vijana wa Hanang, Asia Halamga, kwa niaba ya mkuu wa mkoa misaada kwa waathirika wa mafuriko Hanang.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini, Baraka Ladislaus, akikabidhi misaada hiyo amesema benki hiyo inaungana na familia za wahanga na kutoa misaada ya kibinadamu.

Msaada huo unalenga kutoa faraja na msaada wa msingi ili kusaidia katika kurejesha hali ya kawaida kwa wahanga wa mafuriko.

Mbunge wa Viti Maalumu, Asia Halamga, ameipongeza benki hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii, hasa kwa wahanga wa mafuriko katika kipindi hiki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

error: Content is protected !!