July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NMB yasaidia serikali kukusanya trilioni 8.6

Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania kupitia mifumo yake mbalimbali ya malipo imesaidia Serikali ya nchi hiyo kukusanya Sh.8.6 trilioni kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2019 hadi 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna wakati wa warsha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, wakuu wa wilaya, madiwani, watendaji na waweka hazina.

Zaipuna amesema benki yake imeendelea kuwekeza kwenye teknolojia jambo ambalo limesaidia kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi huku akisisitiza benki yake imejidhatiti kuendelea kutoa bidha zinazokidhi mahitaj ya wateja wake.

“Ubunifu ni kitu pekee ambacho kimetusaidia kupiga hatua na ule uwekezaji ambao tuliufanya kwenye teknolojia ulituwezesha kuwa benki ya kwanza kuunga mifumo yetu na Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) na hadi sasa zaidi ya taasisi 1,100 tayari zimeunga mifumo yake kwenye mifumo ya NMB ya ukusanyaji wa mapato,” amesema.

Zaipuna amesema ukusanyaji wa mapato kupitia mfumo wa kielektroniki umekuwa ukongezeka kutoka 2.1 trilion mwaka 2019 hadi 3.7 trilioni mwaka 2021.

“Fedha hizi zilikusanwa kupitia mifumo yetu ya NMB mkononi, NMB Wakala, Lipa Namba, intaneti nk. Tunaendelea kuwekeza kuhakikisha kuwa mtandao wetu upo vizuri na kuhakikisha usalama wa malipo,” amesema.

Aidha, Zaipuna amesema benki yake imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya jamii nchini kote nakuongeza benki yake kwa makusudi ilizindua taasisi yake ya NMB Foundation ilikuchangia maendeleo endelevu.

Amesema benki yake kwa makusudi iliamua kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka kuchangia maendeleo nchini kote kwenye sekta za elimu, afya, kilimo, mazingira, uwezeshaji na matukio ya dharura.

Zaipuna amesema benki yake itaendelea kushirikana na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo serikali ilikuleta maendeleo chanya na endelevu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameishukuru benki hiyo kwa kuendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali za kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Makalla amesema utendaji mzuri wa benki hiyo umetokana na mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yamewekwa na awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku akisisitizakuwa Serikali itandedelea kuboresha mazingira ya kubiashara ilikuvujia wawekezaji wengi nchini.

“Benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele wa kuchangia shughuli zetu za serikali. Serikali ina hisa kwenye benki hii na juzi tu wametoa gawio kwa serikali. Tutaendela kushirikiana na Benki ya NMB ili kujoresha mazingira ya wananchi wetu,” amesema Makalla.

Ameitaka benki hiyo kuendelea kubuni bidha mbalimbali zinazogusa wananchi kuanzia ngazi ya chini na kusisitiza kuwa Serikali itaendela kuchangia ushirikishwahi wa kifedha yaani financial inclusion.

error: Content is protected !!