Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yapata faida ya kihistoria bilioni 211
Habari Mchanganyiko

NMB yapata faida ya kihistoria bilioni 211

Spread the love

 

BENKI ya NMB nchini Tanzania imevunja rekodi kwa mara nyingine kwa kupata faida ya Sh.211 bilioni baada ya kodi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 42 na ni zaidi ya faida yote ya mwaka 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Faida kabla ya kodi ni Sh.302 bilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 43. Katika robo ya tatu ya mwaka iliyoishia Septemba 2021, benki hiyo imeonesha ufanisi mkubwa na mafanikio katika maeneo mbalimbali ya kimkakati.

Kasi ya ongezeko la mapato iliendelea huku uwekezaji katika maeneo mapya na utekelezaji mipango endelevu ya kidijitali nayo ikiimarishwa pia.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema, matokeo ya kuimarika kiutendaji yameiwezesha benki hiyo kupata faida kabla ya kodi ya Sh.302 bilioni na faida baada ya kodi ya Sh.211 bilioni.

Amesemahili ni ongezeko la asilimia 43 ya faida iliyopatikana kipindi kama hicho mwaka jana na zaidi ya faida ya kihistoria ya mwaka wote wa 2020 ambayo ilikuwa ni kiasi cha Sh.206 bilioni.

“Mkakati wetu wa uendeshaji umeendelea kuwa sahihi huku mafanikio ya kuendeleza umiliki wa soko ukipelekea kupatikana kwa faida kubwa.”

“Tunaendelea bila kuchoka kuzingitia matakwa ya wateja na tumeshuhudia kukua kwa kasi ya ukopeshaji na amana za wateja kwa mwaka huu mzima,” amesema Ruth.

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna

Mtendaji mkuu huyo amesema, katika kipindi cha miezi tisa kufikia Septemba mwaka huu, jumla ya mapato ya NMB yalikuwa ni Sh.721 bilioni, kiasi ambacho ni asilimia 20 zaidi ya Sh.601 bilioni zilizopatikana kipindi kama hicho Mwaka mwaka jana ikichangiwa zaidi na kuongezeka kwa mikopo na miamala.

Amesema, mikakati ya benki ya kudhibiti gharama za uendeshaji imeendelea kuzaa matunda na kusababisha kuboreka kwa uwiano wa matumizi na mapato halisi kufikia asilimia 47 kutoka asilimia 52, kiwango kilicho ndani ya matakwa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) cha asilimia 55. Benki inaendelea kuboresha utendajikazi na uwekezaji hasa kwenye maeneo ya kimkakati.

“Nidhamu ya hali ya juu ya NMB katika kutekeleza mipango yake ya kimkakati imeendelea kuiongezea imani kwa wateja na hivyo na kuifanya iimarike zaidi kwenye nafasi yake ya benki inayoongoza nchini,” amesema

“Tunawashukuru wateja wetu wenye thamani kubwa kwetu, wanahisa, wadau wote na wafanyazi kwa ujumla kwa kuendelea kutuunga mkono.”

“Tunapoelekea kumaliza mwaka wa 2021 tuna matumaini makubwa na safari iliyo mbele yetu na tutaendelea kujitolea kusizadia jamii zote tunazozihudumi,” amesema

Amesema, Mali zote za benki zilikuwa na thamani ya Sh.8.2 trilioni mwishoni mwa Septemba 2021, ongezeko la asimilia 17 (YoY) kutoka Sh.7 trilioni kipindi kama hicho mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!