Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Biashara NMB yamkabidhi Rais Samia vifaa vya mamilioni vya elimu kwa wenye uhitaji
BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yamkabidhi Rais Samia vifaa vya mamilioni vya elimu kwa wenye uhitaji

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameishukuru na kuipongeza Benki ya NMB kwa mchango unaoenda kufanikisha uboreshaji elimu kwa makundi maalum. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni baada ya NMB kumkabidhi Rais Samia misaada mbalimbali yenye thamani ya Sh.58 milioni vikiwemo vya kusaidia kuona na kusikia kwa shule nne za jijini Dar es Salaam.

Rais Samia ametoa poongezi hizo wakati wa ziara maalum katika Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Kariakoo, iliyolenga kufanikisha maboresho mbalimbali ya elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma katika shule za sekondari Benjamin Mkapa, Uhuru Mchanganyiko na Jangwani, na Shule ya Msingi Uhuru Wasichana.

Katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu NMB, Ruth Zaipuna, aliyemkabidhi Rais Samia vifaa maalum 60 vya kusaidia wanafunzi wenye uziwi, vifaa 90 vya kusaidia wenye ulemavu wa macho – vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 24, pamoja na kompyuta mpakato ‘laptop’ 20 zenye thamani ya Sh.20 milioni na vifaa vya michezo vya Sh.14 milioni.

“Serikali imetumia Sh.5.9 bilioni katika uboreshaji elimu ngazi ya awali, msingi, sekondari na vyuo, ili kuhakikisha wenye mahitaji wote wanapata elimu nchini. Nawashukuru sana NMB kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu Ruth Zaipuna, kwa kubeba changamoto za vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule hizi,” amesema Rais Samia

“CEO wa NMB hapa amenikabidhi vifaa vya kusaidia usikivu, uoni na hata kompyuta mpakato 20, ombi langu kwenu ni kutuongezea ‘laptop’ kama hizo kwa sababu shule hizi ni nyingi na mahitaji ya hizo kompyuta ni mengi. Tunawaomba mtusaidie katika hili ili kupunguza changamoto hiyo kwa vijana wetu,” amesisitiza.

 

Awali, Zaipuna alisema: “Mheshimiwa Rais, NMB ni mdau mkubwa wa elimu Tanzania, ndio maana tumekuja hapa kukuunga mkono katika jitihada za Serikali yako za kuhakikisha Watanzania wanapata elimu bora.”

“Tumekuja hapa na vifaa vya kusaidia kuona 90, vya kusaidia kusikia 60, ‘laptop’ 20, pamoja na vifaa vya michezo katika shule hizi.”

“Misaada hii inayolenga kusaidia wanafunzi wa shule hizi, tunaamini itaenda kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zilizoelezwa katika risala ya shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa, huku vifaa vya michezo tukiamini vitasaidia kuboresha michezo kwa ustawi wa afya za wanafunzi wetu katika shule husika,” alisema zaipuna.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, aliitaja NMB kama ‘mkono wa kulia wa Serikali ya mkoa’ wake, kwa namna inavyojitoa kupambana na maboresho kwenye Sekta ya Elimu na miundombinu yake, lengo likiwa kuunga mkono jitihada za kufanikisha elimu bora kwa wanafunzi wa mkoa wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!