Thursday , 7 December 2023
Home Kitengo Biashara NMB yakabidhi mabati ya mil.28 kwa shule 5 Kisarawe
Biashara

NMB yakabidhi mabati ya mil.28 kwa shule 5 Kisarawe

Spread the love

KATIKA kuendeleza utamaduni wa Uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR), Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh28.2 milioni kwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Almasi Nyangassa kwa ajili ya shule tano za msingi za Halmashauri hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Kisarawe, ambako Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, alimkabidhi DC Nyangasa mabati hayo, naye kuyakabidhi kwa Walimu Wakuu wa shule hizo, mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Beatrice Dominic.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa (kulia) akiagana na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper (kushoto) mara baada ya kupokea msaada wa msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule tano za msingi wilayani Kisarawe. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Beatrice Dominic.

Shule zilizonufaika na msaada huo, ambao thamani yake ni sehemu ya asilimia moja ya faida baada ya kodi ya Benki ya NMB kwa mwaka jana, ni Kibasila (bati 200), Titu (bati 100), Panga la Mwingereza (bati 100), Mtunani (bati 100) na Vilabwa (bati 100).

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper, alisema thamani ya mabati hayo ya Sh 28.2 milioni ni sehemu tu ya kiasi cha Sh6.2 bilioni zilizotengwa na benki hiyo kusapoti jitihada za Serikali katika sekta za Elimu, Afya, Majanga na Mazingira kwa mwaka 2023.

“Tuko hapa kukabidhi mabati 200 yenye thamani ya Sh. Mil. 9.4 kwa Shule ya Msingi Kibasila, huku shule za Panga la Mwingereza, Mtutani, Titu na Vilabwa – kila moja tukiikabidhiwa mabati 100 yenye thamani ya Sh4.7 milioni hivyo kufanya jumla kuu kuwa Sh28.2 milioni.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa, akizungumza wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 kutoka Benki ya NMB kwa ajili ya shule tano za msingi wilayani humo. Kushoto ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper na wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Zuberi Kizwezwe.

“Kiasi hiki ni sehemu ya Programu ya Uwekezaji kwa Jamii ambayo NMB tumekuwa tukiifanya kwa zaidi ya miaka saba sasa, ambako kwa mwaka huu peke yake tumetenga Sh6.2 bilioni kusaidia utatuzi wa changamoto zinazokwaza sekta za elimu, afya, majanga na mazingira.

“Mheshimiwa mgeni rasmi, elimu ni miongoni mwa sekta za kipaumbele kwa benki yetu na hii ni kutokana na ukweli kwamba ndio ufunguo wa maendeleo ya taifa lolote duniani, na wanafunzi wanaopata elimu mashuleni wanatokana na jamii iliyotufikisha NMB hapa tulipo,” alisema.

Alibainisha usaidizi wao katika utatuzi wa changamoto za elimu, unalenga kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambayo inapambana kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa elimu bora mijini na vijijini na wao kama wadau, hilo ni jukumu lao.

DC Nyangassa kwa upande wake aliishukuru NMB kwa kujitoa kwao katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi, na kwamba ingawa kutoa kupitia CSR ni utaratibu wa kawaida kwa taasisi hiyo, lakini kwa Serikali ni jambo kubwa linalopaswa kuungwa mkono na wadau wa elimu.

“Mnalofanya hapa NMB ni jambo kubwa sana kwetu, mnaunga mkono juhudi za Serikali ya Rais Samia, ambayo kwa mwaka huu wa fedha,  imetupa kiasi cha Sh443.42 milioni kwa ajili ya maboresho mbalimbali ya miundombinu ya elimu Wilaya ya Kisarawe tu.

“Hii sio mara ya kwanza kwenu, mmefanya hivi kwa kutoa madawati mashuleni, vifaa tiba mahospitalini na zaidi ya yote mlikuwa nasi kuwezesha na kushiriki ‘Programu ya Kisarawesha’, inayolenga kuboresha mazingira ya kiuchumi kwa wanawake wa Kisarawe,” alisema DC Nyangassa.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Fatma Nyangassa (wa tatu kushoto), akipokea sehemu ya msaada wa mabati 600 yenye thamani ya Sh. Milioni 28.2 kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Dismas Prosper (wa tatu kulia), wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa shule tano za msingi wilayani humo. Kulia ni Diwani ya Kata ya Kisarawe, Abel Mudo na wa pili kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Kisarawe, Bertha Mungure.

Alisema yote hayo ni uthibitisho wa moyo wa kujali na kuthamini jamii walionao NMB, huku akiwapongeza Walimu wa shule zilizonufaika na msaada huo, kwa kufanya kazi kwa bidii licha ya ugumu wa mazingira ya kufundishia yanayozikabili shule zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

CEO NMB ashiriki mkutano wa Benki ya Dunia

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ameshiriki...

Biashara

Jisajili Meridianbet kasino msimu huu wa Sikukuu upate mgawo wa Mil 2.5

Spread the love  UNAIJUA 200% inakuaje? Meridianbet msimu huu wa Sikukuu za...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Biashara

GGML yataja mbinu kuimarisha miradi ya ujenzi, Bashungwa atoa maagizo

Spread the loveKATIKA kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuimarisha...

error: Content is protected !!