July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NMB yakabidhi gawio la 16.6/-bilioni

Waziri wa fedha Tanzania Saada Mkuya

Spread the love

BENKI ya NMB imekabidhi gawio la Sh. 16.5 bilioni kwa Serikali ikiwa ni faida iliyotokana na kufanya biashara kwa muda wa mwaka mmoja. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Akikabidhi hundi ya fedha hizo mjini Dodoma leo kwa Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Waziri Barnabas, amesema gawio hilo ni ongezeko la asilimia 16 ikilinganishwa na mwaka jana.

“Mwaka huu benki imepata faida ya Sh. 155.6 bilioni ambapo kila mwanahisa amepata gawio la Sh. 104 kwa kila hisa tofauti na mwaka jana ambapo walipata Sh. 90 kwa hisa,’ amesema.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha aliipongeza NMB kwa gawio hilo na kwamba fedha hizo sio ndogo.

“Wote tunajua kwamba biashara ya benki siyo rahisi, NMB inajitahidi inafanya kazi vizuri na kwa weledi kiasi cha kuweza kupata faida,” amesema.

Ameongeza kuwa, serikali ina hisa asilimia 31 katika benki hiyo na kwamba faida hiyo iliyopatikana itakwenda katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

“Faida hii inamrudia mwananchi kwa kuwa itatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo,”amesema Mkuya.

Wakati huohuo, Kampuni ya Puma Energy Tanzania (Ltd) na yenyewe imekabidhi gawio la Sh. bilioni tatu kwa Serikali lilipotikana katika kipindi cha biashara kwa mwaka 2004.

Akikabidhi hundi ya fedha hizo, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Philipe Corsaletti amesema ni matumaini yake, watatendelea kushirikiana na serikali ambayo inamiliki hisa asilimia 50 kutekeleza malengo waliojiwekea mwaka 2015.

Mkuya alishukuru kwa gawio hilo huku akiipongeza Kampuni ya Puma kwa kuendesha biashara ya mafuta ambayo ina changamoto nyingi na ushindani mkubwa.

error: Content is protected !!