Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yajidhatiti kuendelea kuchangia ukuaji matumizi ya bima
Habari Mchanganyiko

NMB yajidhatiti kuendelea kuchangia ukuaji matumizi ya bima

Spread the love

BENKI ya NMB imesisitiza kuendelea kutoa huduma za bima zinazoendana na matakwa ya wateja ikiwa ni utekelezaji wa dhamira yake ya kuongeza matumizi ya bima nchini kote. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

 Hayo yalisemwa jana tarehe 14 Mei 2023 wakati wa uzinduzi wa semina ya Akaunti ya Dhamana ya Bima (Trust Account) iliyopo chini ya benki ya NMB iliyokutanisha wawakilishi wa makampuni ya bima na Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Bima (TIRA), jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soraga (katikati) akipeana mkono na Afisa Mkuu wa wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao (wapili kushoto) baada ya kufungua semina iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya wawakilishi wa makampuni ya Bima juu ya TIRA “TRUST ACCOUNT” uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, Mkuu wa Idara ya Huduma za Taasisi wa Benki ya NMB, William Makoresho (kulia) na wa pili kushoto ni Naibu Kamishna wa TIRA, Khadija Issa Said.

Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao alisema ni heshima kubwa kwa benki ya NMB kuaminiwa na TIRA na kuwa miongoni mwa taasisi za fedha ambazo zitakazoendesha  akaunti hiyo muhimu kwaajili ya makampuni ya bima nchini.

Shayo alisema uanzishwaji wa Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni hatua nzuri ambayo itasaidia kuimarisha usimamizi wa sekta ya bima kuendana na matakwa ya kisheria na udhibiti yaliyowekwa na TIRA.

“NMB tupo tayari kuwahudumia kwa ueledi na ufanisi mkubwa. Natumia nafasi hii kuomba makampuni mengi ya bima kuendelea kutuamini na kufanya kazi na sisi,” alisema Shao.

Alisema zipo sababu nyingi kwa makampuni ya bima kuridhia kufanya kazi na benki ya NMB zikiwa ni pamoja na ubora wa mifumo ya benki hiyo ambayo inahakikisha upatikanaji wa taarifa na njia bora za mawasiliano kati ya benki, kampuni za bima na TIRA kama wasimamizi na wamiliki wa Akaunti hiyo.

“Uimara wa kifedha tulionao kama benki ya NMB ni sababu nyingine na tayari tunayo timu maalum ya wafanyakazi wa benki ya NMB wenye ueledi kwaajili ya kushirikiana na kufanya kazi na makampuni ya Bima,” alisema.

Naye Dk. Baghayo Saqware Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) alisema chimbuko la Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni Kanuni namba 20 ya Bima ya mwaka 2009 inayozitaka Kampuni za Bima kuweka Amana za Usalama angalau asilimia 50 ya kiwango cha chini cha mtaji halisi wa kampuni husika ya bima.

Alisema uamuzi wa kufungua Akaunti ya Dhamana ya Bima katika benki za biashara ni mwarobaini wa changamoto hiyo huku alisisitiza kuwa TIRA itaweza kusimamia moja kwa moja fedha hizo za amana za akiba, jambo ambalo si tu litaimarisha usimamizi, bali pia kuboresha maendeleo ya sekta ya fedha.

“Malengo nakubwa ya kanuni hiyo ni kuhahkikisha kunakuwepo na raslimali fedha ya kufidia wateja wa bima. Kama kampiuni itafilisika au kufungwa, fedha hizo kutumika kufidia wateja. Kabla ya kuja na kanuni hizi, tuliona changamoto kadha mojawapo ikiwa ni uwezekano wa kukyukwa sheria  kwa watoa huduma,” alisema.

Dk Saqware alisema  mamlaka yake kwa kushirikiana Chama cha Watoa Huduma za Bima (ATI), walikubaliana kuandaa Mwongozo wa Uwekazaji wa Usimamizi wa Ukwasi ambao pia ulielekeza uanzishwaji wa Akaunti ya Dhamana ya Akiba kupitia benki za biashara ili kuondokana na tatizo la changamoto ya kimtaji au kushindwa kulipa fidia za madai ya wateja wake.

“Moja ya masharti ya Akaunti hiyo ya Dhamana ya Bima ni kuwa benki lazima itoe mafunzo na tunashukuru kuwa benki ya NMB imeweza kutekeleza hili,”

Aliipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na huduma za bima huku akiongeza kuwa sekta sekya ya bima imekuwa kwa kasi hivi karibuni.

Naye mgeni rasmi ya warsha hiyo Mudric Ramadhan Soraga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar aliisihi TIRA kuwashirikisha watoa huduma za bima wakati wa utungaji wa sharia na sera mbalimbali za bima.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!