Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yajitosa uwezeshaji watalii kutoka China kutembelea Tanzania  
Habari Mchanganyiko

NMB yajitosa uwezeshaji watalii kutoka China kutembelea Tanzania  

Spread the love

BENKI ya NMB imesisitiza dhamira yake ya kuwa benki chaguo katika kuwezesha watalii kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo China kutembelea Tanzania kwa kutoa huduma za hali ya juu za kibenki na suluhisho zinazokidhi matarajio yao. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Hayo yalisemwa na jana na Afisa Mkuu Rasilimali Watu wa NMB, Emmanuel Akonaay  kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Ruth Zaipuna wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa NMB kwa ushirikiano na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) visiwani Zanzibar kwa mawakala wa usafirishaji na waandishi wa vyombo vya habari kutoka China.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Simai Mohamed Said ( aliyekaa Katikati) katika picha pamoja na wageni kutoka China ambao ni watoa huduma za Utalii na wanahabari waliokuja kwaajili ya kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania, safari ambayo imedhaminiwa na Benki ya NMB. watatu kushoto ni Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay pamoja na viongozi wa ubalozi wa Tanzania nchini China na maafisa waandamizi wa kamisheni ya Utalii Zanzibar.


Akonaay alisema benki hiyo tayari imeshirikiana na wadau mbalimbali kukuza mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii kama sehemu ya juhudi zake za kukuza ukuaji wa haraka na mzuri wa sekta ya utalii.

“NMB inaifahamu vizuri sekta hii ya utalii na mahitaji yake. Tunajua wateja wanahitaji huduma mahususi za kifedha zinazopatikana kwa urahisi pamoja na masuluhisho ya biashara yaliyoundwa mahususi kwaajili yao. Kama benki, tumefanya mengi kuhakikisha tunatoa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja,” alisema Akonaay

Alisema jitihada za kuhakikisha urahisi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya utalii, benki hiyo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China, Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) na Kampuni ya Omnihorizon Group zilianzisha Tantour, jukwaa la masoko ya utalii kwa njia ya mtandao lenye lengo la kushirikisha watalii kutoka mashariki ya mbali hususan China kutokana na ukweli China ina idadi kubwa zaidi ya watalii wanaotoka nje duniani kote.

“Benki ya NMB imejidhatiti kutengeneza uzoefu na kukumbukwa ambayo haitasahaulika kwa watalii kutoka nchini China kuanzia hatua ya kuingia nchini hadi wanapotoka. Tutaendelea kutoa huduma za hali ya juu za benki na masuluhisho katika jitihada za kuunga mkono ukuaji wa sekta ya utalii,” alisema

Alibainisha tayari benki hiyo ina dawati maalum la Kichina la kushughulikia wateja wa China na ina uhusiano mkubwa na benki za China ambazo ni pamoja na ICBC, Benki ya China na Benki ya Mawasiliano.

“Kwa makusudi, hivi karibuni tumeanzisha akaunti maalum ya Yuan ya Uchina (CNY) ambapo wateja wetu wa China wanaweza kupokea CNY nchini China na kutuma CNY kutoka China kutoka ndani na nje. Kama benki namba moja nchini Tanzania, tuna uwezo wa kutoa mikopo na dhamana na kwa mkopaji mmoja sasa tunatoa hadi dola milioni 135 kwa mkupuo moja,” alibainisha.

Alisema NMB ina zaidi ya akaunti 150 za makampuni na biashara, asilimia 96 zikiwa za wawekezaji kutoka China zikiwemo kampuni za serikali, makampuni binafsi na watu binafsi kutoka sekta mbalimbali nchini.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Rahim Bhaloo wakati wa hafla hiyo alisema Zanzibar ni kivutio cha kipekee cha utalii kilicho salama na kuongeza kuwa kisiwa hicho kina miundombinu zote muhimu ikiwemo mahoteli ya kifahari ya kuwahudumia watalii.

“Tuko tayari kupokea watalii kutoka nchini China kuja Zanzibar na tutashirikiana na mawakala wa usafirishaji nchini China ili kukakikisha sote tunapata mafanikio,” alisema.

Awali, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Hafsa Mbamba wakati wa hafla hiyo alisema, “huu ni mwanzo tu wa ushirikiano wetu wenye tija kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na China.”

Mkuu wa ujumbe huo kutoka China Bella Huang, wakati wa hafla hiyo alimwaga sifa nyingi kwa Tanzania kuwa na vivutio vingi vya utalii na kuahidi kuwavutia watalii zaidi wa China kuja kutembelea Tanzania miezi michache ijayo.

“Tumekuwa hapa kwa siku nne tu na tumefurahiya kila kitu. Zanzibar ni nzuri sana na bahari inaonekana poa sana. Tutajitahidi kuhakikisha tunaleta watalii wengi zaidi nchini Tanzania,” alisema Huangng

Mkuu wa msafara wa mawakala wa usafirishaji kutoja China, Bella Huang alimwaga sifa nyingi kwa Tanzania kuwa na vivutio mbalimbali vya utalii  huku akiahidi kuwa kampuni ya wakala wa usafirishaji kutoka China zitawavutia watalii zaidi wa China kuja Tanzania katika miezi michache ijayo.

“Tumekuwa hapa kwa siku nne tu na tumefurahiya kila kitu. Zanzibar ni nzuri sana na bahari inaonekana poa sana. Tutajitahidi kuhakikisha tunaleta watalii wengi zaidi nchini Tanzania hivi karibuni,” Huangng alisema.

Naye Waziri wa Utalii na mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said alisema watalii wanaotarajiwa kutoka Mashariki ya Mbali ikiwemo China mara nyingi waapenda kutafuta na kutembelea maeneo ya kipekee.

“Watalii hawa wakija hapa watapata fursa ya kuona maeneo hayo ya kipekee  ambao wanayoyatafuta. Sisemi kwamba nchi nyingine si nzuri kama Tanzania lakini ukweli ni kwamba sisi Tanzania ni nchi ya kipekee,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!