July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NMB yafadhili wiki ya unywaji maziwa Katavi

Spread the love

 

BENKI ya NMB nchini Tanzania imekabidhi tisheti 300 kwa uongozi wa Mkoa wa Katavi zitakazotumika katika maadhimisho ya wiki ya unywaji maziwa Kitaifa inayofanyikiwa mkoani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Katavi … (endelea).

NMB imekuwa ni sehemu ya maendeleo ya kilimo kwa upande wa uwezeshaji ambapo benki hiyo wamekopesha fedha nyingi kwenye kilimo lakini pia kwenye uvuvi na uzalishaji wa maziwa na ufugaji wa Ng’ombe.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi Berdon Mwakatobe wakati akikabidhi tisheti kwa Katibu Tawala Mkoa wa Katavi (RAS) ambaye alipokea kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki.

Mwakatobe alisema ukiachana na kudhamini maazimisho haya NMB wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo kuliko benki yeyote nchini humo kwa kukopesha fedha nyingi katika sekta za kilimo, mifugo, uvuvi na sekta ya uzalishaji wa maziwa kwa lengo la kuisadia serikali katika kumkomboa mwanachi kuichumi.

Alisema benki hiyo imetoa Sh.100 bilioni ambazo zimekopeshwa kwa asilimia10 na zimekwisha na wameongeza fedha nyingine ambazo kwa sasa zinakopeshwa kwa asilimia 9.

“Fedha zipo kwa ajili yenu wadau wote wa kilimo karibu kwenye Tawi lolote la NMB kupata fursa hii. Wadau waje wajitokeze kukopa kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla,” alisema

Aidha alisema NMB wanaendelea kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo umwagiliaji na sekta ya Tumbaku na sekta nyingine zote za kilimo kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya unywaji maziwa NMB watakuwa wanatoa huduma mbalimbali kwa wateja wao ikiwemo kufungua akaunti kutoa elimuya mikopo ya NMB na kwa ajili ya wajasiliamali.

Kwa upande wake, RAS wa Katavi, Rodrick Mpogolo aliishukuru NMB na bodi ya maziwa kwa kupeleka wiki ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa kitaifa katika mkoa wa katavi.

Alisema mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa yenye mifugo mingi kwani ni ni miongoni mwa mikoa mitano nchini Tanzania yenye idadi kubwa ya mifugo.

Mpogolo alisema Mkoa wa Katavi unamaziwa mengi akini inawezekana uhamasishaji wa unywaji wa maziwa bado upo chini.

“Inawezekana wengi wetu hatutumii maziwa kwani maziwa nilishe na yanaboresha afya zetu ukinywa maziwa umepata mlokamili, bodi ya Maziwa na NMB wameleta kitu muhimu sana kwa wanachi wa mkoa wa Katavi kwa ajiliya maendeleo na usitawi wa kiuchumi na afya kwaajili ya wanachi wa mkoa wa Katavi,” alisema

Naye Mwakilishi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Christerbel Swai aliishukuru NMB kwa kuwa wadau muhimu katika shughuli muhimu kwenye nchi yetu ya Tanzania ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa.Swai alisema shughuli ya uhamasishaji wa unywaji wa maziwa hapa nchini hufanyika kila mwaka mwezi wa sita kwenye shughuli hizo wadau wa maziwa huwa wadhamini wakuu wa shuguli hizi na mwaka huu Benki ya NMB imewadhamini jumla ya Tisheti 300.

error: Content is protected !!