
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Benki ya NMB kwa kuchangia maendeleo visiwani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Ametoa pongeza hizo hivi karibuni wakati akipokea msaada wa mabati 255, mbao 220 pamoja na misumari kilo 100 vyote vikiwa na thamani ya Sh.13 milioni kwa ajili ya kuezekea Kituo cha Afya cha Jang’ombe kilichopo Wilaya ya Mjini Magharibi Mkoa wa Magharibi.
Rais Mwinyi alisema, msaada huo utahochea maendeleo kwa wananchi na kuwaomba wadau wengine kuiga mfano wa NMB.
Naye Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Donatus Richard alisema benki hiyo, imetenga asilimia moja kurejesha kwa jamii ili kusaidia jamii inayaowazunguka katika mambo mbalimbali.
Alisema wameamua kutoa msaada huo baada ya kupokea changamoto hiyo na kugushwa na shida ya wananchi ili kusaidia jamii na kuungana na serikali katika kuleta maendeleao.
Richard alisema, ndani ya miaka miwili benki hiyo imetumia Sh.195 milioni kutoa misaada mbalimbali, ikiwemo vituo vya afya na shuleni.
Aidha, alisema NMB itaendelea kuwa bega kwa bega na wananchi kwa kutoa misaada mbalimbali ambayo itasaidia jamii inayowazunguka, ambapo pia aliwataka wananchi kuendelea kujiunga na benki hiyo.
More Stories
Huduma ya Teleza Kidigitali yazinduliwa Morogoro
Taasisi yaanzisha mafunzo kuwanoa wadau wa mawasiliano nchini
GGML yatoa msaada wa magari manne VETA Mwanza