Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania imetangaza rasmi kuanza kupokea maombi ya ufadhili wa masoko kwa wanafunzi wa kidato cha tano na wa vyuo vikuu nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Uzinduzi huo umefanywa leo Alhamisi, tarehe 19 Mei 2022 na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB Foundation, Ruth Zaipuna mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

“Maana yake ni kwamba, leo tumefungua rasmi dirisha la kupokea maombi ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotegemea kuingia kidato cha tano mwaka huu pamoja na wale watakao ingia vyuo vikuu mwaka huu kwaajili ya masomo ya shahada zao za kwanza,” amesema Ruth.

“Kupitia ‘Nuru yangu Scholarship and Mentorship Program’ tunaenda kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wenye uwezo lakini wanatoka kwenye mazingira magumu,” amesema.

Afisa mtendaji mkuu huyo amesema, kwa kuanzia, mwaka huu watatoa ufadhili kwa wanafunzi 200 – tunaanza na kidato cha tano wa mwaka huu – 2022/2023 ambao tutachagua wanafunzi 150 na wanafunzi wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023 watakuwa 50.

Amesema, ufadhili wa gharama za elimu kwa masomo ya kidato cha tano na sita kwa shule za serikali zitahusu ada, nauli za kwenda na kurudi, vifaa vya shule, fedha za kujikimu, bima ya afya, na gharama zingine kama itakavyo ainishwa kwenye fomu ya kujiunga na shule, “mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa daraja la kwanza alama saba mpaka 14.”

“Masomo ya shahada ya kwanza zitahusu ada, fedha za kujikimu, fedha kwaajili ya mafunzo kwa vitendo, gharama zote zinazolipwa kwa chuo, vifaa vya shule na komputa mpakato. Mwanafunzi lazima awe na ufaulu wa daraja la kwanza alama tatu,” amesema.

Amesema mbali ya ufadhili kwa kulipia gharama, Programu ya Ufadhili ya NMB Nuru Yangu Scholarship and Metorship program itatoa ufadhili pamoja na usimamizi maalum yaani (mentorship) ambayo itachangia maendeleo kamili ya wanafunzi kitaaluma na kinidhamu.

“Ufadhili huu mbali na uwezo wa mwanafunzi, lakini pia utazingatia fani za hesabu na takwimu, biashara, uchumi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), uhandisi, uhasibu, mafuta na gesi, sayansi na udaktari wa binadamu,” amesema.

Kuhusu ‘Mentorship’ au mpango wa usimamizi kwa walengwa wetu amesema, katika kipindi cha masomo yao, wanafunzi hao watapewa walezi ambao watawasaidia kuwasimamia na kufuatilia maendeleo kamili ya masomo yao hatua kwa hatua kwa kuhimiza ubora wa kitaaluma, nidhamu, kukuza uongozi na kufahamu umuhimu na utamaduni wa kurudisha kwa jamii.

“Kwa ufadhili huu wa elimu kupitia NMB Nuru Yangu Scholarship and Mentorship Program, tunatarajia kuibua vipaji vya vijana na kuwasaidia kufikia ndoto zao kupitia teknolojia na mabadiliko ya fikra, tabia, uongozi, uzalendo, ujasiriamali ili waweze kutengeneza ajira mpya, kujiajiri au wawe wanaajirika,” amesema.

Amesema ili kuomba ufadhili huu, unatakiwa kufika kwenye tawi lolote la NMB na lililopo karibu yako,utapatiwa fomu ambayo utaijaza na kuirudisha hapo hapo ulipoitoa. Pia fomu hizi zinapatikana kwenye mtandao kupitia foundation.nmbbank.co.tz.

Aidha, amesema ili kuwapata wanafunzi kweli wanaotoka mazingira magumu, “tutashirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na wadau wengine ili kuhakikisha hasa tunapata wanafunzi wenye uhutaji.

Pia, Ruth ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB amesema, wanaanza na idadi hiyo ya wanafunzi 200 huku wakiendelea kuzungumza na kutafuta wadau wengine ili kupanua wigo zaidi ya wanufaika katika siku za usoni.

3 Responses

  1. Most of Tanzanian student who live in difficults if may not meet the division of point 3 in advance and 7 to 14 in o level what is you view

  2. Naomba maelekezo namna ya kutuma maombi ya ufadhili na sifa za mwombaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *