October 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NMB kurejesha milioni 246 kwa wananchi

Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania, imetenga Sh.246 milioni zitakazotumika kununua na kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali wa promosheni ya Bonge la Mpango. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). 

 

Promosheni hiyo awamu ya pili, ilizinduliwa mwishoni mwa wiki na

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki hiyo, Filbert Mponzi, makao makuu yake jijini Dar es Salaam.

 

Mponzi alisema washiriki wa poromeshi hiyo ni wateja wapya watakaofungua akaunti na kuweka fedha kuanzia Sh.100,000 au kuhamisha Sh.100,000 kutoka kwenye benki zingine na wateja wa zamani watakaoongeza fedha kwenye akaunti zao.

 

Alisema, kutakuwa na zawadi mbalimbali kama fedha taslimu kuanzia Sh.100,000 na pikipiki za miguu mitatu aina ya Toyo 50 zitakazokuwa zikitoka kila wiki.

 

“Benki ya NMB imeendelea kurudisha faida kwa jamii na sasa imetenga Sh.246 milioni ambazo zitatumika kununua zawadi mbalimbali,” alisema Mponzi

 

“Sisi tunataka kuendelea kufanya benki hii namba moja nchini iendelee kuwa salama kwa suluhisho lingine kwa Watanzania wote. Wateja wote ambao wako na sisi na wale wapya, tutaendelea kuwaletea promosheni za kutosha,” alisisitiza

 

Aidha alisema, kati ya Toyo hizo 50 ambayo moja ni Sh.4.4 milioni, Desemba pekee ambayo itakuwa mwisho wa promosheni hiyo, zitatengwa Toyo 14  zenye tahamani ya Sh.62 milioni “ambazo hizi zitatolewa ndani ya mwezi huo.” 

 

Aidha, Mponzi alitumia fursa hiyo kuwaomba wakulima kufungua akaunti katika benki hiyo ili fedha wanazozipata au kulipwa kutokana na mauzo ya mazao yao ipitie maeneo sahihi na yenye usalama.

 

“Katika kipindi hiki cha mavuno, tunawashauri wakulima kufungua akaunti ili malipo yao yapitie kwenye benki yetu ambayo imesambaa maeneo yote nchini. Lakini nji moja wapo ya kuingia moja kwa moja kwenye promosheni hii,” alisema

error: Content is protected !!