July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NMB kukusanya mapato ya halmashauri nchini

Spread the love

BENKI ya NMB ipo katika mpango wa kuunganisha huduma za kielektroniki za ukusanyaji mapato katika halmashauri zote nchini ili kuondoa mianya ya rushwa kwa baadhi ya watendaji, anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Richard Makungwa, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Serikali NMB amesema, lengo la kuunganisha huduma hizo ni kuongeza mapato katika halmashauri ili kuchochea maendeleo ya jamii.

“NMB kwa kutambua umuhimu wa halmashauri katika utoaji wa huduma za kijamii ambapo hufanikisha kazi hizo kutokana na mapato yanayopatikana kupitia vyanzo vya ndani, tumeanza kuunganisha huduma za kielektroniki za ukusanyaji mapato,” amesema Makungwa.

Amesema kuwa, NMB itaendela kufanya maboresho ya huduma hizo ili kuhakikisha halmashauri zinakusanya kodi inavyostahili, kuweza kupata bajeti toshelezi itakayosaidia kuifikishia jamii huduma zinazostahili.

“NMB ni mkusanyaji mkuu wa mapato ya halmashauri zote, watumishi wengi wa serikalini hufanya shughuli za kibenki katika benki yetu. Tunawajibu wa kuhakikisha kuwa serikali na Halmashauri tunazisaidia kulinda mapato yake,” amesema.

Pia, Benki ya NMB imetoa msaada wa Sh. 100 Mil kwa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambazo zitatumika kutekeleza shughuli mbalimbali za Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika Aprili 7-9, 2016 mkoani Dodoma.

“Tumekubali kuudhamini mkutano wa ALAT ili kuiendeleza desturi yetu ya kusaidia mikutano yao mikuu ya uchaguzi ili kuwapata viongozi wapya wa Jumuiya hiyo,” amesema.

Makungwa amewataka wadau wengine kujitokeza kuudhamini mktano huo kwa kuwa kiasi kilichotolewa hakitoshelezi mahitaji ya mkutano huo.

error: Content is protected !!