June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nkrumah yafanywa kumbukumbu ya taifa

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu

Spread the love

UKUMBI wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo umetangazwa kuwa “sehemu rasmi ya kumbukumbu ya taifa.” Anandika Pendo Omary … (endelea).

Mbali na ukumbi huo kijumuishwa katika maeneo ya kumbukumbu ya kihistoria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia kitakuwa ni sehemu ya kumbukumbu ya historia ya taifa.

Lazaro Nyarandu – Waziri wa Maliasili na Utalii, ndiye aliyetangaza na kusaini hati ya utambuzi wa ukumbi huo kuwa sehemu rasmi ya kumbukumbu ya taifa wakati wa tamasha la saba la Mwalimu Julias Nyerere linaloendelea chuoni hapo.

Nyarandu amesema, “leo natangaza rasmi ukumbi huu wa Nkrumah unakuwa sehemu rasmi ya kumbukumbu ya taifa. Unakuwa ni jengo na eneo namba 228 lililohifadhiwa kisheria.”

“Ukumbi huu una historia kubwa na nyeti ya taifa. Ni ishara ya uhuru tulionao wa majadiliano ya wazi yanayotokana na tafiti mbalimbali ikiwemo kupanuka kwa demokrasia,” amesema Nyarandu.

Ameongeza kuwa, kama ukumbi huo utabadilishwa ni lazima vigezo na utaratibu wa kisheria vifuatwe.

Aidha, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala amesema tangu ukumbi huo ujengwe mwaka 1960 umekuwa ukitumiwa na marais, mawaziri, wanaharakati na vikundi vya ukombozi kutoka ndani na nje ya nchi hasa bara la Afrika.

“Kulingana na heshima ya matumizi yaliyotukuka ya ukumbi huu, ndipo tukaona ni vizuri jengo la ukumbi huu litambulike kama tunu ya taifa. Na mchakato wa kulihifadhi, kulilinda na kuliendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo, ulianza miaka mitatu iliyopita kwa kuiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kulitambua,” amesema Mukandala.

error: Content is protected !!