May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nkamia aanguka uchaguzi Simba

Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba

Spread the love

 

ALIYEKUWA Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia ameangukia pua kwenye uchaguzi wa klabu ya Simba baada ya kushindwa na Murtaza Mangungu kwa tofauti ya kura 472 katika uchaguzi mdogo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akitangaza matokeo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Klabu ya Simba, Boniface Lihamwike amesema kuwa idadi ya kura zilikuwa 1,140 na kati ya hizo kura zilizohalibika ni nane.

Katika kura hizo Nkamia alipata jumla ya kura 330 sawa na asilimia 28.95, huku Mangungu akipata kura 802 sawa na asilimia 70.35 na kutangazwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti.

Uchaguzi huo uliokuwa unafanyika kujaza nafasi ya mwenyekiti ilioachwa wazi na Swedy Nkwambi aliyejiuzuru wadhifa huo tarehe 14 Septemba 2019.

Mara baada ya kutangazwa matokeo hayo, Nkamia aliwashukuru wanachama kwa kura walizompa na kuahidi kushirikiana na Mangungu katika kutekeleza majukumu yake.

“Nawashukuruni sana kwa kura zote mlizonipa na nimpongeze ndugu yangu kwa kuchaguliwa na nakuhakikishia nitakuunga mkono kuhakikisha Simba inapata ubingwa mwaka huu,” alisema Nkamia.

error: Content is protected !!