February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Njombe yatikiswa, mtoto mwingine auawa

Ruth Msafiri, Mkuu wa Wilaya ya Njombe

Spread the love

MTOTO mwingine mwenye umri wa miaka Saba (7), ameuawa leo tarahe 2 Februari, kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana wilayani katika eneo la Lupembe, wilayani Njombe, mkoani humo, kwa madai ya imani za kishirikishirikiana. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa wilaya hiyo, Ruth Msafiri, ameeleza kuwa mwili wa mtoto huyo umekutwa umetelekezwa kwenye kichaka cha Lupembe. Amesema, mtoto huyo aliuawa kikakitili wakati akirejea nyumbani kwao kutokea shuleni.

Mauaji haya yanatokea siku tatu tangu serikali kulieleza Bunge, kuwa watu wanaojihusisha na mauwaji ya watoto katika eneo la Njombe kwa tuhuma za kishirikina, tayari wameshakamatwa.

Kauli ya serikali ilikuja katikati ya shinikizo la wananchi lililotokana na watoto Sita kuuwawa ndani ya kipindi cha wiki moja na baadhi ya viungo vyao kukatwa.

Akizungumza bungeni Ijumaa iliyopita – tarehe 31 Januari, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alisema, tayari “wauwaji wamekamatwa” na mauwaji kukomeshwa.

Waziri Lugola alitoa maelezo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kaskazini, Menrad Kigola, aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali kushughulikia tatizo hilo.

Mauaji hayo ya kikatili, yaliyozua taharuki kubwa katika mikoa ya kusini mwa Tanzania, yanaelezwa kuwa yanatokana na kuwapo kwa imani potofu za kishirikina.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mkuu wa mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, amekiri kuwa serikali imeelemewa kufuatia kuuawa kwa manafunzi huyo ambaye sasa idadi ya waliouawa imefikia Saba.

Sendeka anasema, serikali itaanza kuwashughulikia matajiri ambao baadhi yao wanashukiwa kuhusika; na au kuchochea kuwapo kwa mauaji hayo kwa ajili ya kujipatia kipato cha haraka.

“Tutaanza na matajiri ambao wanaaminika wanapata utajiri kwa njia haramu. Hawa tutawashika ili walisaidie Jeshi la Polisi katika kufanya upelelezi ili kuwapata wahusika,” ameeleza Sendeka.

Siku za hivi karibuni kumeibuka vitendo vya kuuwawa watoto wadogo vinavyofanywa na “watu wasiojulikana” katika nyakati tofauti katika eneo hilo.

Wote waliouawa mpaka sasa, miili yao imepatikana ikiwa imetolewa baadhi ya viungo kama vile meno, masikio, na viungo vya siri.

error: Content is protected !!