Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Njama za kumnyima mshahara wa ubunge Lissu hizi hapa
Habari za SiasaTangulizi

Njama za kumnyima mshahara wa ubunge Lissu hizi hapa

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

KUNA njama zinasukuwa na ofisi ya Bunge za kutomlipa mshahara, posho na stahiki nyingine, mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka Dodoma … (endelea).

Lissu yuko Ubelgiji kwa takribani miezi 10 sasa, kufuatia kushambuliwa kwa risasi, nje ya nyumba yake, Area D, mjini Dodoma. Alikuwa akirejea nyumbani kutokea bungeni.

Mwanasiasa huyo ambaye ni Mnadhimu wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni na mwanasheria mkuu wa Chadema, anapatiwa matibabu na madaktari bingwa wa mifupa katika hospitali ya chuo kikuu cha Luvein, kilichopo nchini humo.

Lissu alikwenda kwenye matibabu nchini Ubelgiji, tarehe 6 Januari mwaka jana.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wanaoitwa na serikali, “watu wasiojulikana,” akiwa nyumbani kwake area D Jijini Dodoma. Kabla ya kufkikishwa Ubelgiji, mwanasiasa huyo machachari wa upinzani, alitibiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma na Nairobi nchini Kenya.

Njama za kumnyima Lissu stahiki zake, zimeonekana wazi leo Alhamisi, bungeni mjini Dodoma, baada ya mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku Msukuma, kumuomba Spika kusitisha haki zake.

Alisema, “leo tunajadili taarifa za kamati ya wizara ya afya na kwa kuwa zipo sheria za kutambua mtu kuitwa mgonjwa, Lissu tulijua kuwa ni mgonjwa. Lakini leo tunaona akizurula huko Ulaya akilitukana Bunge na serikali.”

Alisema, “leo tunajadili taarifa za kamati ya wizara ya afya na kwa kuwa zipo sheria za kutambua mtu kuitwa mgonjwa, Lissu tulijua kuwa ni mgonjwa. Lakini leo tunaona akizurula huko Ulaya akilitukana Bunge na serikali.”

Mara baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu, Msukuma aliomba mwongozo wa kutaka Lissu asilipwe mshahara na posho kwa madai kuwa hajulikani kama bado anaumwa au ameshapona. Mwongozo wa Msukuma ulionekana kuwafurahisha baadhi ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi.

Akijibu mwongozo wa Msukuma, Spika Ndugai alisema, anakubaliana na hoja hiyo kwa kuwa Lissu anaonekana anazunguuka ulimwenguni “kuchafua serikali.”

Alisema, “ni kweli, kwamba jambo la Msukuma juu ya Lissu linahitaji kuangaliwa kipekee. Mbunge hayupo bungeni; hayupo jimboni na hayupo Tanzania. Spika hana taarifa, hakuna taarifa ya madaktari wake. Lakini yeye anaonekana anazunguuka ulimwenguni.”

Aliongeza: “Hoja ina msingi ya kusimamisha malipo yake hadi hapo tutakapo pata taarifa zake. Hatujui kama anaumwa. Kwa maelezo ya Msukuma anasema, anazurula. Nikuhakikishie haya mambo yapo ndani ya uwezo wangu.”

Taarifa zinasema, watu waliotaka kuondoa uhai wa Lissu, walitumia magari mawili – Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol yenye Na. T 932 AKN.

Tokea mwishoni mwa mwaka jana, Lissu ameanza ziara ya kutembelea nchi za Ulaya, ikiwamo Ujerumani na Uingereza. Juzi alizuru nchini Marekani ambako amekuwa akishiriki mijadala mbalimbali juu ya utawala bora, uhuru wa kujieleza, haki ya kutoa na demokrasia.

Katika safari yake hiyo, Lissu alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha BBC; baadaye akazuru nchini Ujerumani na kufanya mahojiano na runinga ya DW. Kwa sasa, Lissu yupo nchini Marekani na ameshafanya mahojiano na runinga ya VoA.

Kote huko, Lissu ameendelea kusisitiza kuwa serikali ya Rais John Pombe Magufuli, ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake. Amelishambulia Bunge chini ya Spika Job Ndugai kwa ‘kumtelekeza’ na kushindwa kulipia matibabu yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!