August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Niyonzima kuwakosa Al-Ahly

Spread the love

HARUNA Niyonzima ataukosa mchezo wa kwanza wa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati kikosi chake cha Yanga kitakapovaana na Al-Ahly ya Misri Aprili 9, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, anaandika Kelvin Mwaipungu.

Kiungo huyo mshambuliaji wa Yanga, ataukosa mchezo huo muhimu, baada ya kupata kadi mbili za njano mfululizo katika michezo dhidi ya APR.

Wakati Niyonzima anaukosa mchezo huo, lakini kuna hatihati nyota wengine wa kutumainiwa na Yanga wakaukosa mchezo wa marudiano kama wakipata kadi ya njano katika mechi dhidi ya Al-Ahly.

Wachezaji hao ni washambuliaji Donald Ngoma na Amissi Tambwe ambao wote kwa pamoja walipata kadi katika mchezo dhidi ya APR uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hivyo wachezaji hao wanatakiwa kuwa makini katika mchezo wa kwanza dhidi ya Al-Ahly ili kuepuka kupata kadi nyingine ya njano ambayo itapelekea kukosa mechi ya marudiano itakayochezwa kati ya Aprili 15 na 16 jijini Cairo, Misri.

error: Content is protected !!