Rais Samia Suluhu Hassan amesema ataizindua mwenyewe miradi yote inayotekelezwa Wilayani Chato mkoani Geita kama ambavyo angefanya mtangulizi wake Hayati Dk. John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Rais Samia ameyasema hayo leo Alhamis tarehe 17 2022 katika maadhimisho ya kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kuondoka kwa kiongozi huyo wa Serikali ya awamu ya tano.
“Kwa hapa Chato naomba niwahakikishie kwamba miradi yote tuliyopanga na ambayo tumeshaanza kuitekeleza itakamilika nafahamu pia ujenzi wa kivuko cha Chato Hapa Kazi Tu, kimeshakamilika kwa asilimia 100 na kimegharimu Sh 3.1 bilioni, vilevile ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato umefikia asilimia 95 kwa gharama ya Sh 58.9 bilioni.”
“Stendi mpya ya Chato iliyogharimu Sh 13 bilioni imefikia asilimia 90 na mabasi madogo yameshaanza kuingia naomba niwaahidi wana Chato, miradi yoye ikikamilika nitakuja kuizindua mwenyewe kama ambavyo angefanya Dk. Magufuli angekuwepo,” amesema Rais Samia
Aidha amesema “nimearifiwa Hospitali ya Rufaa ya kanda inayojengwa kwa Sh 34 bilioni, unaendelea vizuri na baadhi ya huduma zimeanza kutolewa. Niwahakikishie tutakamilisha yote hata ile midogo ambayo sijaitaja hapa.”
Leave a comment