January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Niqab kupigwa marufuku Uingereza

Spread the love

WAZIRI wa Elimu wa Uingereza, Nicky Morgan ameeleza kuunga mkono taasisi za elimu nchini humo kutokana na mapendekezo yao ya kutaka vazi la Niqab kupigwa marufuku nchini humo.

Hatua hiyo inaelezwa kuungwa mkono kutokana na kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini humo kwa kile kilichoelezwa kuwepo kwa ama kushamiri kwa mashambulizi ya kigaidi duniani kote.

Taasisi hizo zimeeleza kwamba, ni vema kupigwa marufuku kwa vazi hilo kwenye shule zote nchini humo ikiwa ni hatua za awali za kutambuana tofauti na sasa ambapo vazi hilo linavaliwa.

Akizungumzia kuunga kwake mkono Morgan ameeleza kuwa, kupigwa kwa marufuku hiyo kunaweza kutekelezwa kwa wanafunzi na walimu.

Wakati Uingereza ikielekea kuipigia chapua hoja hiyo, Ufaransa tayari imepiga marufuku si vazi la niqab pekee bali hijabu (vazi la kuhifadhi mwili kwa mwanamke).

Wazirii Mkuu wa Uingereza, David Cameroon akizungumzia hisia hizo amesema, hataki nchi hiyo kuwekwa hiyo ya kupiga marufuku vazi la hijabu kama ilivyo Ufaransa.

Pamoja na kauli hiyo, ameeleza kuunga mkono taasisi pamoja na idara za kielimu zilizopiga marufuku uvaaji wa niqab.

error: Content is protected !!