February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nini kimetokea uchaguzi marudio udiwani

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage

Spread the love

KATIKA hali ya kawaida mtu anaweza kujiuliza nini kimetokea katika uchaguzi wa marudio katika kata 43 hapa nchini.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa kawaida kwamba maisha yamezidi kuwa magumu, anaandika Richard Makore.

Licha ya malalamiko hayo, lakini uchaguzi wa marudio uliofanyika jana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimenyakua viti 42 na kuviacha mbali vyama vya upinzani.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimejinyakulia kata moja licha ya wananchi kushuhudia umati mkubwa katika mikutano yao ya kampeni.

Bado kuna maswali mengi kuhusu matokeo hayo lakini ukweli ni kwamba yameishatangazwa.
Kata hizo 42 ni pamoja na Bomambuzi, Mnadani, Machame Magharibi, Weruweru, Kijichi, Mbweni, Saranga, Muungano na Mhongozi

Zingine ni pamoja na Majengo, Milongodi, Chipogoro, Muriet, Reli, Makiba, Moita, Musa, Maroroni, Mnacho, Kitwiru, Ambureni, Maloloni, Legeruki, Ngabobo, Nata na Siuyu.

Kata zingine ni pamoja ni Bonyokwa, Mhandu, Kimala, Senga, Kalulu, Kijima, Bukwimba, Lukumbile, Chanikanguo, Lunguza, Mamba, Nangwa, Kiloka, Ndalambo, Chikonji, Sumbawanga asilia na Ibhigi ambayo Chadema imeibuka na ushindi.

error: Content is protected !!