October 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Nimeitwa kuitumikia Chadema

MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Morogoro, James Samson Mabula (Power Mabula) akiwa Jukwani akimwaga Sera za Chadema.

Spread the love

MCHUNGAJI wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Morogoro, James Mabula, amesema ameitwa na Mungu kukitumikia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaandika Bryceson Mathias, Morogoro… (endelea).

Akizungumza katika mikutano ya uhamasishaji na ujenzi wa chama baada ya kutia nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Morogoro Mjini, Mabula alisema “nilipata wito wa kukitumikia Chadema katika Siasa na kujiunga nacho mapema kabisa, kwa sababu ndicho chama pekee nilichoona kina nia ya dhati ya kuwakomboa Watanzania.”

Mabula amesema “baada ya kuona udhaifu wa baadhi ya wabunge wengi wa CCM na wale wa upinzani ambao hawako katika Ukawa, nimepata wito wa kutia nia ya kugombea ubunge Morogoro.”

Amefafanua kuwa, endapo atapitishwa na kushinda ubunge, kazi yake kubwa itakuwa ni kuhakikisha anarudisha kwa wananchi viwanda 11 vilivyouawa na serikali ya CCM mkoni Morogro.

Mabula ametamba kuwa hatua hiyo itakwenda sambamba na kuhakikisha huduma ya maji inavifikia kata zote 29 za Manispa ya Morogoro.

Hadi sasa makada 11 wa Chadema wametanagaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, linaloongozwa na Abdul-Aziz Mohamed Abood (CCM).

error: Content is protected !!