July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nigeria yazisaidia kaya maskini Tanzania

Spread the love

SERIKALI ya Nigeria imeelezea kufurahishwa na mpango wa kunusuru kaya maskini kwa kuzipatia ruzuku, ambao unatekelezwa na serikali ya Tanzania, kupitia Mfuko wa Maendeleo wa TASAF. Anaandika Dany Tibason, Chamwino … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa juzi na kiongozi wa msafara wa wajumbe 20 kutoka serikali ya Nigeria, Peter Pafka walipotembelea wilaya ya Chamwino, kijiji cha Wiliko, kujifunza jinsi mpango huo unavyotekelezwa.

Pafka amesema wamefurahishwa na jinsi serikali ya Tanzania ilivyopiga hatua kubwa katika mpango wa kunusuru kaya maskini kwa kuwapa ruzuku ambayo imeweza kuwasaidia wananchi wake kijiongezea kipato.

“Tangu tumefika hapa juzi tumetembelea baadhi ya vijiji vilivyopo kwenye mpango huo, tumejionea jinsi wananchi walivyoweza kushirikishwa katika na kuweza kuzitumia fedha hizo kwa malengo husika,” amesema.

Amesema ujumbe huo wa kunusuru kaya maskini kutoka Nigeria walivutiwa kuja kujifunza Tanzania kuhusu mfuko wa Tasaf ulivyoweza kufanikiwa katika kupunguza umasikini kwa wananchi.

Aidha amesema nchi yao wameingia kwenye mpango huo wa kunusuru kaya maskini na katika Afrika Tanzania ndiyo imefanikiwa katika mpango huo.

Naye Mkurugenzi wa Uratibu wa Tasaf nchini, Alphonce Kyariga amesema kwa sasa Mfuko huo, upo katika hatua ya tatu ambayo inawashirikisha kaya maskini kufanya miradi ya maeneo yao kwa kutoa nguvu kazi na kuwalipa fedha.

Kyariga amesema katika mpango huo wananchi wa maeneo husika wamekuwa wakifanya shughuli za maenedeleo kama ujenzi wa barabara katika maeneo yao na mfuko huo kuwawezesha kwa kuwalipa fedha za kufanya mradi huo.

Alisema katika mpango huo kila kaya maskini inawakilishwa na mtu mmoja katika kazi za mradi wa maendeleo kila siku lakini kwenye malipo anakabidhiwa aliyeandikishwa kwenye mpango.

Aidha Mkurungenzi huyo aliwasihi wananchi waliopo kwenye mpango huo, kuzitumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuinua kipato cha kaya hizo maskini kama Serikali ilivyolenga kuwasaidia.

error: Content is protected !!