Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Nigeria yafungia mtandao wa Twitter
Kimataifa

Nigeria yafungia mtandao wa Twitter

Spread the love

 

NCHI ya Nigeria, imefungia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa muda usiojulikana, ikijibu mapigo baada ya mtandao huo kufuta taarifa ya Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uamuzi huo ulitangazwa jana Ijumaa, tarehe 4 Juni 2021 na Waziri wa Habari wa Nigeria, Lai Mohammed, siku mbili baada ya mtandao huo kufuta chapisho la Rais Buhari.

Waziri huyo alisema, Serikali ya Nigeria imechukua hatua hiyo, kupinga uamuzi huo wa Twitter, kwa madai kwamba ulikua sio sahihi.

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, Jumamosi ya leo tarehe 5 Juni 2021, baadhi ya watu nchini Nigeria wameshindwa kufungua mtandao wa Twitter , hasa wanaotumia simu, huku wanaotumia kompyuta wakifanikiwa kuingia.

Jumanne ya tarehe 1 Juni 2021, mtandao wa Twitter ulifuta chapisho la Rais Buhari, kwa madai kuwa, lilikiuka kanuni za mtandao huo. Chapisho hilo lilibeba ujumbe wa kuwaonya vijana wanaohamasisha baadhi ya mikoa ya Kusini Mashariki ya Nigeria kujitenga.

Katika chapisho hilo, Rais Buhari aliwaonya wapingaji hao kwamba atawachukuliwa hatua, akisema kwamba wanataka kuleta machafuko nchini humo.

Huku akikumbushia madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyoibuka Nigeria kuanzia mwaka 1967 hadi 1970

“Wengi waliofanya utovu wa nidhamu leo ni wachanga sana kufahamu uharibifu na upotezaji wa maisha ya watu, uliotokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe Nigeria. Wale tuliokuwa mashambani kwa miezi 30 ambao tulipitia vita, tutawashughulikia kwa lugha wanayoielewa.” aliandika Rais Buhari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Papa Francis kukutana na wahanga wa vita Sudan Kusini

Spread the love  KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis leo Jumamosi...

Kimataifa

Polisi ahukumiwa kifo kwa kumuua wakili

Spread the love  MAHAKAMA kuu nchini Kenya imemhukumu kifo Ofisa wa Polisi,...

Kimataifa

Hospitali za China zilifurika wagonjwa, wazee kipindi cha wa likizo ya Mwaka Mpya wa Lunar

Spread the loveHOSPITALI  nchini China zimejaa wagonjwa na wazee katika kipindi cha...

Kimataifa

Papa Francis ayataka mataifa ya nje kuacha kupora mali DRC

Spread the love  KIONGOZI wa kanisa Katoliki Papa Francis, ameyataka mataifa ya...

error: Content is protected !!