Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NIDA watakiwa kuongeza ofisi za kutoa vitambulisho
Habari Mchanganyiko

NIDA watakiwa kuongeza ofisi za kutoa vitambulisho

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Steven Kebwe ameiagiza ofisi ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoa, kuongeza vituo vya  kutolea huduma katika wilaya zote ili kuwasaidia wananchi hasa waishio vijijini  kupata huduma hiyo kiurahisi. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mkuu huyo wa mkoa alisema hayo jana wakati alipotembelea ofisi hizo kufuatia malalamiko yaliyotolewa kwake na wananchi juu ya kuchelewa kupata namba pamoja na vitambulisho jambo linaloleta athari za usajili wa laini za simu kwa jamii.

Alisema, licha ya zoezi hilo kuonekana likiendelea kufanywa lakini bado miezi minne tu kusitishwa kwa zoezi la usajili wa laini za simu kwa alama za vidole hapo mwezi Desemba mwaka huu, huku watu wengi wakiwa bado hawajapata.

Aidha aliitaka jamii kuwa na mwamko wa kuitumia nafasi iliyopo ya kwenda kupata huduma hiyo kwa wakati kwani kuchelewa kunaweza kuleta usumbufu baadae.

Naye John Msekwa mkazi wa Tungi alisema, serikali za mitaa zinatakiwa kuchukua nafasi yake kwa kuwatambua wakazi wa maeneo husika ili iwe rahisi kwao kupata vitambulisho bila kutegemea masharti yaliyopo.

“Nina miaka ya kuzaliwa zaidi ya 70 hapa, cheti nakipata wapi kwa sasa na nina mwezi wa sita natuafuta kitambulisho, kitambulisho changu cha kupigia kura  kimeharibika sana, kila ninapokwenda wanagoma kunisajilia laini,” alisema.

Akizungumzia hilo Afisa Usajili wa vitambulisho NIDA mkoani hapa, James Malimo alisema kuchelewa kwa upatikaji wa vitambuliso hivyo kwa baadhi ya wananchi kunatokana na wananchi wengi kushindwa kutimiza masharti yaliyowekwa na kwamba yapo maombi mbalimbali yamekwama kutokana na changamoto za wananchi kushindwa kuwasilisha vielelezo zaidi.

Hivyo aliwaasa wananchi kuhakikisha wanakamilisha masharti hayo ya vielelezo vya msingi na kuhakikisha wanavipata kwa wakati ili kuweza kukamilisha usajili na maombi yao yafanyiwe kazi kwani hawataweza kumsajili mtu bila kuwa na vielelezo ili kuepuka kuwasajili wasio watanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!