Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Nida kupunguza utitiri wa vitambulisho
Habari Mchanganyiko

Nida kupunguza utitiri wa vitambulisho

Spread the love

 

MAMLAKA ya Uzalishaji wa Vitambulisho vya Taifa (Nida) nchini Tanzania, imeanza kushughulikia tatizo la kupunguza utitiri wa vitambulisho kwa kuongeza thamani ya kitambulisho wanachotoa kwa kuanza kutengeneza vitambulisho aina ya ‘Smart Card.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lengo ni kumwezesha mwananchi kutumia kitambulisho hicho watakachokuwa wanakitoa siku za usoni kupata huduma mbalimbali kwenye maeneo tofauti kama ya umeme, bima, maji, usafiri na kwenye taasisi za kifedha.

Hayo yalisemwa juzi Jumamosi tarehe 18 Machi 2022 na Mkurugenzi wa Nida, Edson Guyai wakati akizungumza kwenye mdahalo wa kujadili mwaka mmoja wa utawala wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kurushwa na Azam TV.

Pia, taasisi zingine zilizoshiriki kwenye mdahalo huo ni, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Guyai alisema miongoni mwa malengo ni kumpunguzia mzigo mwananchi wa vitambulisho na tayari wameanza kuunganisha mifumo yake ya utambuzi wa ikolojia kwa taasisi zaidi ya 50 za kiserikali na binafsi ili kutatua changamoto hiyo.

Alisema wanataka ifike wakati raia wakienda kwenye taasisi yeyote waulizwe swali ambalo hajawahi kuulizwa sehemu yoyote, “kama vile unaulizwa jina, kwa hiyo sisi tunampango wa kutoa vitambulisho vya smart card, kwa kuviongezea thamani, tunataka kitambulike kama ATM, bima na au kama taarifa yeyote ambayo itamwezesha raia kupata huduma yeyote ya kijamii atakapokwenda.”

Kuhusu mafanikio waliyoyapata ndani yam waka mmoja, alisema wamefanikiwa kusajili watu milioni moja na kutoa namba ya utambulisho kwa wananchi milioni 1.3, kutoa vitambulisho milioni tatu na kufanya mamlaka tangu ianzishwe mwaka 2013 imesajili raia milioni 22.8 na namba ya vitambulisho milioni 19.2 na kutoa vitambulisho milioni 10.7 pamoja na kugawa vitambulisho milioni 9.6 milioni.

Aidha, Guyai alisema malengo waliyojiwekea ni kuboresha mifumo yao ya Tehama ili kuhakikisha mwananchi anajisajili mtandaoni akiwa sehemu yoyote kisha anabakisha kupeleka baadhi ya nyaraka pekee pamoja na kuwekas alama ya kidole tofauti na sasa mhusika anapaswa kufika ofisini na kuandikishwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema wamefanikiwa kuongeza idadi ya wanufaika wa mikopo na sasa wanafanya mapitio upya ili kuangazia maeneo yenye changamoto kama kiwango cha fedha wanachokitoa.

Aidha, akijibu swali la fedha kuwa kiduchu pamoja na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati kama VETA, Badru alisema wamesikia kilio hicho, “na tunafanya mapitio makubwa na kuangalia jinsi ya kuwawezesha hawa wa vyuo vya kati na kama tunavyosema yajayo yanafurahisha.”

Mkurugenzi wa Bodi MIkopo ya Elimu ya Juu, Abdul-Razaq Badru

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Hosea Kashimba alisema, ndani yam waka mmoja wa Rais Samia umekuwa furaha kwa wastaafu kwani mafao yao yamelipwa na sasa wanaboresha mifumo yao ili kuhakikisha wastaafu wanapata mafao yao mapema iwezekanavyo.

Kashimba alisema, miongoni mwa maboresho ni kuanza kutumia mifumo ya teknolojia kwa wastaafu kuwa na utaratibu wa kuhakikiwa kupitia simu zao za mkononi, “kwa hiyo mtu anaweza kidole gumba popote atakapokuwa, kwa hiyo ukiweka kidole unaingiziwa fedha na usipoweka hela haiingii. Yaani tunataka tusiwe tunakutana nao bali tunaonana kimtandao mtandao tu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!