August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NICOL yazidi kupaa, yajipanga kuwekeza kwenye madini, gesi

Moja ya kituo cha gesi asilia

Spread the love

KAMPUNI ya NICOL Investment (PLC), imeendelea kupata faida na hisa zake kuendelea kufanya vizuri katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa hesabu zilizokaguliwa za kampuni hiyo, faida yake imepanda kutoka Sh. 1.5 bilioni mwaka 2020 mpaka Sh. 4 bilioni mwaka 2021.

Hisa za Kampuni hiyo kwenye soko la hisa nazo zimeonekana kuendelea kupanda kwa kasi kutoka Sh. 200 mwaka 2020 hadi Sh. 360 mwaka huu.

Akizungumzia siri ya mafanikio hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NICOL, Erasto Ngamilaga, amesema ni kweli mapato ya kampuni hiyo ya kizalendo yanaendelea kupaa kwa kasi.

Amesema wakati kampuni hiyo inasajiliwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam mwaka 2018 ilikuwa na changamoto nyingi sana lakini “kwa sasa mambo yako safi na wanahisa wanafurahia kampuni yao kuendelea kufanya vizuri” huku wakilipwa magawio na kupata taarifa za kampuni kwa uwazi.

Ametaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni kampuni kufanya mikutano ya kila mwaka na kwa mfululizo kuanzia mwaka 2018 wanahisa kuendelea kupata gawio la faida mfululizo.

Eraso amesema hivi karibuni walitangaza hesabu zilizokaguliwa zinazoonyesha kuwa faida ya kampuni hiyo imekua kutoka Sh bilioni 1.5 mwaka 2020 hadi bilioni 4 mwaka 2021

Amesema hiyo ni sawa na ongezeko la zaidi ya asilimia 144 na kwamba mafanikio hayo yamechangiwa na mapato wanayopata kutoka kwenye magawio na mapato yanayotokana na riba baada ya kufanya uwekezaji kwenye hati fungani.

error: Content is protected !!