Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Ni vikumbo vita ya usajili
Michezo

Ni vikumbo vita ya usajili

Fiston Mayele mshambuliaji maya wa Yanga
Spread the love

 

IKIWA Ligi Kuu Tanzania Bara imemalizika na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF), limeshafungua dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza, klabu za Azam Fc, Yanga pamoja na Simba zimeonekana kupigana vikumbo katika kuwania saini za wachezaji. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Dirisha hilo la usajili litadumu kwa siku 42, kuanzia tarehe 19 Julai 2021 na litafungwa tarehe 31 Agosti, 2021.

Usajili wa klabu hizo ni katika kujiimalisha kuelekea msimu ujao wa mashindano 2021/21, unaotarajiwa kuanza mwezi ujao, ukizingatia timu hizo zitashiriki michuano ya kimataifa mara baada ya Tanzania kupata nafasi nne za uwakilishi.

Siku ya Jumamosi Julai 31 mwaka huu, Azam Fc ilifanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji raia wa kidemokrasia ya Congo Idri Mbombo, huku klabu ya Yanga ikimpokea mpachika mabao wa klabu ya AS Vita Fiston Kalala Mayele ambao siku za hivi karibuni ataingia mkataba na timu hiyo yenye mskani yake jijini Dar esa Salaam.

Idris Mbombo, mshambuiaji Mpya wa Azam FC

Usajili wa Mbombo kwenye klabu ya Azam Fc, utakuwa umefikisha idadi ya wachezaji watano huku wanne wakiwa wa kigeni ambao wamesajiliwa na klabu toka kufungulia kwa dirisha hilo la usajili kutoka ndani ya bara la Afrika.

Waliosajiliwa mpaka sasa ndani ya kikosi cha Azam Fc ni kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa KenyaKenneth Muguna, aliyeingia kandarasi ya miaka miwili na kiungo mwengine wa kimataifa wa Zambia Charles Zulu ambaye pia amemwaga wino wa miaka miwili.

Kwa upande wa klabu ya Yanga ambao wao mpaka sasa wameshakamilisha usajili wa beki wa kulia kutoka Jamhuri ya kidomokrasia ya Congo Shaban Djuma, kwa mkataba wa miaka miwili, Fiston Mayele ambaye alitua jana nchini kwa ajili ya kukamilisha dili hilo.

Khalid Aucho

Aidha pia Yanga mpaka sasa imeshamalizana na mshambulaji wao wa zamani Heritier Makambo, ambaye atatua nchini muda wowote kuanzania sasa kukamilisha usajili wake.

Licha ya kusubiri kukamilisha usajili wa Makambo lakini pia klabu hiyo, usiku wa Jumamosi ulimpokea kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Msumbuji aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya UD Songo Jimmy Julio Ukonde, ambaye nae amekuja kumalizana na mabingwa hao wa kihistoria.

Simba nao hawakonyuma kwenye vikumbo vya usajili kwa wachezaji hawa wa kimataifa ambao, inaripotiwa kuwa klabub hiyo imeshavungua mazungumzo na kiungo wa kimataifa wa Uganda Khalid Aucho ili kuangalia uwezekana wa kumwaga wino kwa mabingwa hao watetezi.

Kama Simba wakifanikiwa kunasa saini ya kiungo huyo fundi, huwenda wakampa mkono wa kwa heri mchezaji wake mwandamizi Jonas Mkude, ambaye amesimamishwa ndani ya klabu hiyo kwa utovu wa nidhamu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!