July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NHIF yadhamini matibabu ya wachezaji Ligi Kuu

Spread the love

MFUKO wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa klabu 16 vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofnayika leo ofisi za TFF zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amesema wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia klabu za Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.

Tumekua na kilio cha muda mrefu juu ya klabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini klabu zilikuwa zinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.

Naye Mkuu wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote yatakayofnayika ndani ya nchi.

Mchezaji au kiongozi pindi atakapopata tatizo la kuumwa, basi ataweza kutibiwa katika hospitali yoyote yenye huduma ya Bima katika eneo alilopo, lengo ni kuhakikisha wanakua na afya njema kwa ajili ya kushiriki vizuri mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom.

Lengo letu ni kuona wachezaji wanapata huduma ya afya popote wanapokuwa na kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Ligi Kuu, na kuweza kuzitumikia vyema timu zao kwenye mashindano.

Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kwa niaba ya klabu vya Ligi Kuu amesema wanashukuru kupata udhamini huo wa bima ya afya, uwepo wa NHIF umevipunguzia klabu mizigo wa matibabu na sasa klabu zitaweza kushiriki vizuri kwenye michuano ya msimu huu.

error: Content is protected !!