Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko NHC yashusha neema kwa watumishi Mabarali
Habari Mchanganyiko

NHC yashusha neema kwa watumishi Mabarali

Spread the love

HALMASHAURI ya wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya imesema kuwa ili kupunguza adha ya Nyumba za kuishi kwa Watumishi wa Halmashauri hiyo,Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo limepitisha azimia la kununua nyumba 20 zenye thamani ya shilingi Milioni 990 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), anaandika Ester Macha.

Uamuzi huo umepitishwa katika kikao cha robo ya nne ya mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa Maji uliopo Rujewa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ambapo walisema nyumba hizo zitapangishwa kwa watumishi ili waishi jirani na vituo vyao vya kazi.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Mganga Ngumuo amesema Halmashauri iliandika barua kwa Shirika la Nyumba mwaka 2016 ikiomba kuuziwa nyumba ambapo uongozi wa shirika ulikubaliana na ombi hilo.

Ngomuo amesema Halmashauri na Shirika la nyumba wameingia mkataba kwa Halmashauri kulipa fedha taslimu Sh. milioni 50 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na kwamba kiasi kitakachobaki kitalipwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka sita hadi deni litakapokamilika.

Ameongeza kuwa Halmashauri itakuwa ikilipa milioni 196 kwa mwaka kwa nyumba 20 ambazo zitakuwa na vyumba vitatu kila moja ili kuweza kupunguza adha kwa watumishi wake kwani asilimia kubwa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutokana na ukosefu wa makazi bora eneo la Igawa na Rujewa.

Mkurugenzi huyo amesema nyumba hizo zitakuwa msaada kwa watumishi kwani pia zitakuwa zimezungukwa na huduma zote za msingi ikiwemo Hospitali ambapo Shirika linatarajia kuzikabidhi kwa Halmashauri baada ya mkataba kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Francis Mtega amesema uwepo wa nyumba hizo itakuwa sehemu ya mapato kwa Halmashauri kwa kuwa watumishi watakuwa wakilipia pango kama wapangaji wengine.

Amesema kuwa mpango huo kwa halmashauri utakuwa mzuri katika kuongeza mapato yake ndani ya halmashauri na hata urahisi kwa watumishi kutokana na kuwa karibu na vituo vya kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!