March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NGO’s zapigwa ‘stop’ Burundi, kisa ushoga

Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi

Spread the love

TAASISI na Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Burundi yamesitishwa kutoa huduma katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu, yakituhumiwa kuchochea ushoga na vita. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa hiyo ilitolewa jana tarehe 28 Septemba 2018 na Jenerali Silas Ntingurigwa, Katibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Burundi.

Jenerali Ntingurigwa alisema kuwa, Serikali ya Burundi imepiga marufuku baadhi ya mashirika hayo kwa madai ya kukiuka sheria za nchi hiyo.

Naye Jean Claude Karerwa, Msemaji wa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza alisema hatua hiyo imechukuliwa baada ya mashirika hayo kubainika kuingiza tabia ambazo ni kinyume na mila ya nchi hiyo ikiwemo ushoga na kuchochea vita.

error: Content is protected !!