Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko NGO’s zapigwa msasa ukwepaji makosa ya utakatishaji fedha, ugaidi
Habari Mchanganyiko

NGO’s zapigwa msasa ukwepaji makosa ya utakatishaji fedha, ugaidi

Spread the love

 

MASHIRIKA Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) 40, yamepewa mafunzo kuhusu ukwepaji makosa ya utakatishaji fedha na ufadhili wa vitendo vya ugaidi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kwa kushirikiana na Taasisi ya Haki za Binadamu Afrika Mashariki (EAHRI) na Taasisi ya Defenders Protection Initiative (DPI), kutoka nchini Uganda.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema mafunzo hayo yatasaidia NGO’s hizo kutojihusisha na shughuli zinazohamasisha makosa hayo ambayo yako kinyume cha sheria.

“Asasi 40 zimekuja kujifunza madhara yanayokuta asasi wanapoingia kwenye mtego wa kusafisha fedha chafu. Wakati mwingine imetokea zipo taasisi zinashiriki bila kujua au kwa kujua kutakatisha fedha kama za dawa za kulevya na rushwa,” amesema Olengurumea na kuongeza:

“Tuna mkakati kama taiga kuhakikisha tunapambana na utakatishaji fedha na kufadhili ugaidi, hivyo asasi tunaopata fedha ndani na nje ni vizuri kujua zinatoka wapi sababu Kuna vyanzo vichafu.”

Naye Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Msajiki wa NGOs, Denis Bashanga amesema 2018 Serikali ilitoa kanuni Na. 609 inayosimamia masuala ya uwazi na uwajibikaji ili kuhakikisha mashirika hayo hayajiingizi katika vitendo vya utakatishaju fedha na kufadhili ugaidi.

“Kanuni hizi zinalenga kuhakikisha NGO’s na asasi za kiraia zinafanya kazi kwa kuzingatia malengo ambayo nchi inayakubali lakini ambayo yatakuwa siyo kinyume cha dheria. Mashirika yanatakiwa yaweke wazi fedha wanazopata zinakuja kufanya kitu gani na zinatoka wapi,” amesema Wakili Bashanga.

Hata hivyo, Wakili Bashanga amesema hadi sasa hakuna NGO’s au asasi zilizobainika na makosa ya utakatishaji fedha au kufadhili vitendo vya ugaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Usajili wa NGO’s Zanzibar, Mwanabaraka Saleh Sheikha, ameyataka mashirika hayo kutumia mafunzo wanayopata kuepuka makosa hayo.

Mwezesha wa mafunzo hayo ya siku mbili kutokana nchini Uganda, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa DPI, Wanjala Yona, amesema mafunzo hayo yanalenga kukwepesha hatari ya makosa hayo katika usalama wa nchi.

Amesema mafunzo hayo yanalenga kuziwesha NGO’s kutimiza majukumu yao kwa kufuata misingi na sheria za nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

Habari Mchanganyiko

Yara yaja na bima ya mazao kwa wakulima

Spread the love  WAKATI serikali ikiweka mikakati mbalimbali kuimarisha sekta ya kilimo...

error: Content is protected !!