Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari NGO’s zamuahidi Rais Samia mambo 18
HabariTangulizi

NGO’s zamuahidi Rais Samia mambo 18

Spread the love

 

ASASI za Kiraia (AZAKI) na Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), nchini Tanzania, zimemuahidi mambo 18, Rais wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, ili kumuunga mkono katika Serikali yake.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ahadi hizo zimetolewa leo Jumatatu tarehe 29 Machi 2021, mkoani Dar es Salaam na Onesmo Olengurumwa, wakati anasoma tamko la AZAKI la kumpongeza Rais Samia, kwa kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, akichukua mikoba ya Hayati John Pombe Magufuli.

Rais Samia aliapishwa tarehe 19 Machi 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, kufuatia kifo cha Dk. Magufuli, kilichotokea katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, tarehe 17 Machi 2021.

Mratibu huyo wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) amesema, mambo hayo 18 yakitekelezwa, yataisaidia Serikali ya Rais Samia kukuza uchumi wa nchi na wananchi, kulinda katiba na sheria, pamoja na kuimarisha utawala bora na haki za binadamu.

Onesmo Olengurumwa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)

Olengurumwa ametaja mambo hayo ni, kulinda katiba, haki za binadamu, utawala bora na kuishauri Serikali na wadau mbalimbali kuhusu uboreshwaji wa usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi.

Mengine ni, kuchangia ukuaji uchumi wa nchi kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na fedha za AZAKI hizo na kuongeza miradi ya ubunifu na yenye tija kwa jamii na makundi mbalimbali kama vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na watoto.

“Katika taarifa iliyotolewa na Asasi za Kiraia katika wiki ya Asasi za Kiraia tarehe 7 Novemba 2019, mashirika 16 yaliyofanyiwa utafiti yalionyesha yameingiza nchini Sh. 236 bilioni katika kipindi cha miaka mitatu tu (2016-2018) kwa ajili ya kutelekeza miradi mbalimbali nchini,” amesema Olengurumwa.

Mambo mengine ni, kuwajengea uwezo wa kifikra na kiuchumi wananchi kupitia elimu na miradi mbalimbali ya kujenga uwezo itakayofanywa na asasi hizo.

Hali kadhalika, AZAKI hizo zimeahidi kushirikiana na Rais Samia katika kuweka mikakati ya namna ya kuzalisha nafasi za ajira, ili kuondoa changamoto ya uhaba wa ajira kwa vijana.

Pamoja na kufanya kazi zao kwa uwazi na weledi kwa kufuata miongozo ya serikali pamoja na kulipa kodi inavyostahiki.

AZAKI hizo zimeahidi kuchangia ongezeko la utawala bora katika taasisi za kiserikali kutokana na ufuatiliaji utakaoendelea kufanywa na AZAZKI na wadau mbalimbali wa utawala bora na haki za binadamu.

Jambo lingine ambalo asasi hizo zimeahidi kushirikiana na Serikali ya Rais Samia ni kutokomeza umasikini kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekeleza, sambamba na kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma kwenye maeneo mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Saluhu akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa

“Jambo lingine ni kuishauri serikali katika mambo ya msingi yanayohusu usimamizi wa sekta ya AZAKI hapa nchini ikiwemo kuweka mazingira wezeshi ili sekta ya Asasi za Kiraia kukua na kustawi kama ambavyo Ilani ya CCM 2020-2025 ilivyoahidi,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema, AZAKI hizo zitaendelea kumshauri Rais Samia pamoja na Serikali namna ya kusimamia utumishi wa umma kwa mujibu wa matakwa ya taratibu na misingi ya sheria za nchi.

“Tunaahidi kuendelea kuishauri maboresho ya sheria mbalimbali kandamizi ikiwemo namna bora ya kuimarisha utawala bora,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema, AZAKI zinaahidi kuendelea kuvishauri vyama vya siasa kuweka utaratibu wa kupata na kutambua uwakilishi Bungeni wa asasi hizo.

Pia, AZAZI hizo zimeahidi kuendelea kulinda amani ya nchi kwa kuwashauri wananchi namna ya kutunza na kuienzi amani iliyopo.

“Tutaendelea kushauri viongozi, wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mambo muhimu yatakayoweza kuboresha amani ya taifa letu kwa mujibu wa Katiba na Sheri za nchi yetu,” amesema Olengurumwa.

Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Bob Wangwe, amemuomba Rais Samia akutane na asasi hizo, ili wajadiliane namna watakavyoshirikiana kutekeleza ahadi hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari za SiasaTangulizi

Wabunge wacharuka kukatika kwa umeme

Spread the loveTATIZO la kukatika kwa umeme kila mara katika maeneo mbalimbali...

Habari za SiasaTangulizi

Watu 1,673 wamchangia Lissu Sh. 20 milioni kununua gari

Spread the loveWATU 1,673 wamechanga fedha zaidi ya Sh. 20 milioni kwa...

Habari MchanganyikoTangulizi

11 wafariki dunia baada ya mtambo wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar kupasuka

Spread the loveWATU 11 wamefariki dunia huku watatu wakijeruhiwa katika ajali ya...

error: Content is protected !!