Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari NGO’s 20 zajitosa sakata la Ngorongoro, zaomba uwazi, tume huru
HabariHabari Mchanganyiko

NGO’s 20 zajitosa sakata la Ngorongoro, zaomba uwazi, tume huru

Spread the love

 

MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), 20 zinazojishughulisha na masuala ya utetezi wa haki za binadamu, yameomba mgogoro wa ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro, ushughulikiwe kwa uwazi huku wakihimiza uundwaji wa tume huru ya kutafuta suluhu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumamosi, tarehe12 Februari 2022, kupitia tamko la mashirika hayo lililosomwa jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, akishirikiana na  Edward Porokwa, Mkurugenzi wa Pingos Forum.

Akisoma tamko hilo, Olengurumwa ameishauri Serikali iunde tume huru itakayowahusisha wafugaji  wenyeji wa Wilaya ya Ngorongoro, wataalamu wa hifadhi, watetezi wa haki za binadamu na waday wengine, ili ifanye utafiti kuhusu hoja zinazobishaniwa kwa ajili ya kuja na mapendekezo yatakayozingatua ulinzi wa hifadhi na haji za wananchi.

“Sheria inayounda Mamlaka ya Uhifadhi ya Ngorongoro (NCAA),  ipitiwe upya na kuboresha usisimamizi na ulinzi wa haki za wananchi, pamoja na kuhakikisha hifadhi inalindwa na kuendelezwa,” amesema Olengurumwa.

Mratibu huyo wa THRDC, ameikumbusha Serikali kuzingatia malengo matatu ya uanzishwaji hifadhi hiyo, ambayo yalikuwa ni uhifadhi, kulinda maslahi ya wenyeji walioondolewa kwenye Mbuga ya Serengeti kwa mkataba wa wakoloni na utalii.

“Maslahi haya matatu yaliingizwa katika sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, wakati wa wakoloni na yameendelea kuwepo katika sheria ya sasa ya mamlaka ya Hifadhi  ya Ngorongoro,” amesema Olengurumwa.

Hata hivyo, Olengurumwa amesema kama muafaka wa mgogoro huo hautapatikana, kisha wananchi kutakiwa kuondoka, walipwe fidia itakayowasaidia kumudu maisha kwenye maeneo mapya.

“Wananchi  wapewe fidia kubwa  sababu katika matumizi  ya ardhi mseto wale wananchi wanazuiwa kufanya maendeleo ya ardhi, walinyimwa kujenga majengo makubwa, kumhamisha mtu katika mazingira hayo utatumia mazingira gani kumpa fidia? maana yake ni nini, hata namna ya kumpa fidia iwe tofauti na inayotolewa kawaida,” amesema Olengurumwa na kuongeza:

“Kuhamisha watu katika fidia, nadhani wananchi wataumia, ukitumia thamani ya  kilichopo kwenye ardhi wengine wataondoka na 1,000,000, 200,000 na  wengine wasiondoke na kitu. Endapo itafikia hatua hiyo kitu ambacho kitatakiwa kuwa shiiriki ni namna ya kutoa fidia.”

Naye Porokwa, ameshauri suala hilo lijadiliwa kwa uwazi ili ukweli kujulikana kwa ajili ya kupata suluhu ya haki.

“Anayetuhumiwa  ana fursa ya kuzungumza, nadhani kuna kitu hakijakaa sawa, ndicho tunachokiomba kama watetezi wa haki binadamu, kila upande upate fursa ya kusikilizwa ili kujua ukweli. Majibu ya anayetuhumu na kutuhumiwa yawekwe hadharani ili itolewe hukumu ya haki,” amesema Porokwa na kuongeza;

“Ukienda kuongea chumbani wananchi hawatajua nini kinachozungumzwa, kila kitu kiwekwe hadharani ili  wananchi wajue na dunia ione haki imetendeka kwa kila mmoja, hilo ndilo tunalosema lifanyike.”

NGO’s zilizotoa tamko hilo ni pamoja na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC),Taasisi inayotoa msaada kwa Jumuiya ya Wafugaji wa Asili,  THRDC, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Haki Ardhi, Haki Madini, Taasisi ya Kutetea Rasilimali.

Nyingine ni, Taasisi ya Msingi wa Ushirikishwaji Jamii (FCI-Tanzania),Taasisi ya Mipango ya Jamii ya Kijani na Wakala wa Maendeleo Nguruka (NDA).

Mgogoro huo wa muda mrefu uliibuka tena hivi karibuni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, kutangaza nia ya Serikali kutaka kuchukua eneo la ardhi ya vijiji vya Loliondo, lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1500, kwa ajili ya shughuli za uhifadhi.

Aprili 2021, NCAA ilitoa maelekezo ya kuwaondoa baadhi ya wananchi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, wanaodaiwa kuwa wahamiaji haramu.

Kiini cha mgogoro huo inadaiwa kuwa, idadi ya  wananchi wanaoishi katika hifadhi hiyo pamoja na mifugo yao imeongezeka, kitendo kinachodaiwa kuhatarisha usalama wake, ikiwemo wanyama pori kupotea.

Hata hivyo, jamii za wakazi wa Ngorongoro wanapinga madai hayo wakidai si kweli, kwa kuwa wao wamekuwa  wakiihifadhi hifadhi hiyo na wanyama pori. Lakini pia wao si wavamizi sababu waliwekwa hapo kisheria baada ya kuhamishwa kutoka Hifadhi ya Serengeti, miaka ya 1950.

Mgogoro huo kwa sasa umeshika kasi hadi kufikia hatua ya kuibuka bungeni jijini Dosoma, ambapo hivi karibuni  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,   alisema Serikali itawasilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya uanzishwaji NCAA.

Pia, Serikali itatuma  timu  yake kwenda  kuzungumza na wanachi wa maeneo hayo, ili kupata suluhu huku akihidi haki za binadamu zitalindwa katika mchakato huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!