August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ng’ombe wafundishwa kusafirisha magendo

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limebaini mbinu mpya inayotumiwa na baadhi ya wahalifu kwa kusafirisha bidhaa za magendo na kukwepa kodi, wakitumia Ng’ombe, anaandika Peindo Omary.

Katika taarifa ya wiki ya utendaji wa jeshi hilo iliyotolewa na Hezron Gymbi, Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema wahalifu wameendelea kutumia maarifa na mbinu mbalimbali za kuukwepa mkono wa dola.

“Katika operesheni kabambe ya kuwasaka wahalifu sugu jijini Dar es Salaam, tumebaini watuhumiwa wanabadili mbinu za wizi na ukwepaji kodi kwa kuwatumia wanyama kama Punda na Ng’ombe waliofundishwa kwaajili ya kusafiridha bidhaa za magendo,” amesema.

Gymbi amedokeza kuwa katika msako ulioendeshwa na jeshi hilo tarehe 17 mwezi huu eneo la Mbweni katika ufukwe wa bahari ya Hindi, walikamatwa Ng’ombe wakiwa wamebeba vitu mbalimbali zikiwemo televisheni, sukari na sabuni, vyote vikiwa havijalipiwa ushuru.

“Wanayama hao huswagwa ufukwe wa bahari na moja kwa moja kuelekea kwenye boti ambayo imeegeshwa kwenye maji ambako mzigo hupokelewa ili kusafirishwa.

Mizigo inapakiwa kwenye trela la ng’ombe na kuswagwa kwa kupigwa fimbo na ng’ombe hao hukimbia na kupeleka mzigo mahali ambapo wahalifu wanahitaji,” amesema Gymbi.

Aidha, Gymbi amesema jeshi hilo linaendelea kuwasaka wamiliki wa wanyama hao huku akiwataka raia wema kuendelea kutoa taarifa.

 

error: Content is protected !!