Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari
BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love

 

SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa bandari nchini Tanzania kati ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na kampuni ya DP Wolrd ya Falme za Kiarabu, umechukua sura mpya, kufuatia Spika wa Bunge, Tulia Akson, kudai kuwa chombo hicho, bado kinapokea maoni kutoka kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza bungeni leo asubuhi, tarehe 8 Juni 2023, Dk. Tulia Akson alisema, Bunge bado linaendelea kupokea maoni ya wadai kuhusu azimio la Bunge la kuridhia mkataba kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Dubai.

Alisema, “…tarehe 6 Juni 2023, Bunge lilipokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, waliofika bungeni kuwasilisha maoni yao.

“Pamoja na kwamba Bunge lilipokea maoni hayo siku hiyo, bado linaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau kupitia posta na barua pepe. Madai kuwa Bunge tayari imesharidhia azimio hilo, siyo ya kweli.”

Hata hivyo, wakati Spika Tulia akisema, Bunge bado linaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau juu ya suala hilo, taarifa kutoka Dodoma zinaonyesha kuwa tayari kamati zilizopewa jukumu la kusimamia suala hilo, zimeshakamilisha kuandaa mapendekezo yake.

Aidha, kauli ya Spika Tulia imetolewa takribani siku tatu baada ya kinachoitwa, “mapendekezo ya Kamati ya Bunge kuhusu Azimio la mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania,” kuzagaa kwenye vyombo vya habari.

Kwa takribani siku tatu sasa, kumeibuka mjadala mzito kuhusiana na mkataba unaodaiwa umefungwa kati ya serikali na kampuni ya DP World (DPW), kutoka Falme za Kiarabu, huku baadhi ya wadau wakionekana wazi kupinga ukodishaji huo.

Baadhi ya maeneo ambayo wananchi wanayapinga, ni pamoja na ukodishaji huo kutokuwa na ukomo; ukodishaji na uendelezaji kuhusisha bandari zote za Tanzania Bara na mkataba kusheheni mapungufu  yanayohatarisha mustakabali wa taifa.

“Hakuna hakuna anayebisha juu ya haja ya kuboresha bandari zetu. Hakuna anayehoji uwezo na uzoefu wa DP kuendesha na kusimamia bandari ulimwenguni.

Kinachohojiwa ni mafanikio ya nchi zilizoingia mkataba na DPW, mafanikio yake, yametokana na mikataba ya aina hii,” amehoji mmoja wa wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

error: Content is protected !!