July 31, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ngawaiya wa CCM aiomba ‘poo’ mahakama

Spread the love

 

JONATHAN Mulinga, wakili mtetezi katika kesi inayomkabili Thomas  Ngawaiya, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, ameiomba mahakama isogeze mbele kesi hiyo ile amalizane na upande wa mashtaka nje ya mahakama, anaandika Faki Sosi.

 Ngwaiya amefikishwa katika mahakama hiyo ya Hakimu  Mkazi Kisutu kwa kosa la kufanya shughuli za ujenzi wa ghorofa kinyume cha sheria namba 17 kifungu 22(4) ya ukandarasi ya mwaka 1997.

Mulinga amemuomba Respecious Mwijage, Hakimu Mkazi asogeze mbele kesi hiyo ili kujadiliana kwa kupata muafaka nje ya mahakama hiyo.

Respicios Mwijage amekubali ombo hilo ambapo kesi hiyo imesogezwa mbele hadi terehe 16 Juni mwaka huu.

 

error: Content is protected !!