January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ngassa arudi kwa kasi, akitungua Mtibwa mbili

Mrisho Ngassa (kushoto) akipiga saluti kushangilia bao lake la kwanza akiwa na Simon Msuva

Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa jana amerudisha heshima yake katika klabu hiyo baada ya kuifungia mabao mawili katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliomalizika kwa ushindi wa mabao 2-0. Anaripoti Erasto Stanslaus ……. (endelea).

Ngassa ambaye amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza, jana alikuwa shujaa baada ya kuingia katika dakika ya 53 akichukua nafasi ya Kpah Sherman raia wa Liberia na kufunga mabao hayo mawili.

Kwa ushindi huo Yanga imelipa kisasi kwa kuichapa Mtibwa baada ya katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo, Mtibwa iliichapa Yanga kwa idadi hiyo mjini Morogoro.

Kwa ushindi huo sasa Yanga imekwea kileleni kwa kuwa na pointi 25 ikiiacha Azam yenye 22, lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Dakika hiyohiyo aliyoingia, Ngassa alipiga mpira uliogonga mwamba wa juu. Dakika mbili baadaye aliandika bao la kwanza baada ya krosi safi ya chinichini ya Simon Msuva kumfikia Amissi Tambwe, akiwa langoni, akashindwa kuunganisha. Yeye akaimalizia kazi hiyo.

Kama hiyo haitoshi, dakika ya 62, Ngassa alifunga bao la pili kwa kumchambua kipa Said Nduda baada ya pasi safi ya kupenyeza ya Haruna Niyonzima.

error: Content is protected !!